EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 18, 2013

Mambo 15 yanayoweza kuifanya ndoa yenu ikawa imara milele!

Nawapenda sana na nitaendelea kuwapenda katika siku zote za maisha yangu. Hii yote ni kwasababu mmekuwa mkiniunga mkono katika kazi zangu ambazo nimekuwa nikiziandika kupitia safu hii.
Mpenzi msomaji wangu, maisha ya ndoa ni matamu na utamu wake unakuja pale unapobahatika kuwa na mtu uliyetokea kumpenda na yeye akaonesha kukupenda kwa dhati pia.

Lakini pia wataalam wa mambo ya kijamii wanaeleza kuwa, siku za mwanzo za maisha ya ndoa huwa matamu sana kiasi cha kila mmoja kuomba kifo kisingekuwepo ili waweze kuishi maisha hayo ya raha milele. Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa, kadiri siku zinavyosogea uimara na utamu wa ndoa kwa walio wengi hupungua na kuonekana kama vile ilikuwa nguvu ya soda.
Hii inatokana na baadhi ya watu kutojua mambo ambayo yanaweza kuifanya ndoa ikabaki kuwa ya furaha kwa muda mrefu. Wiki hii nimekuandalia mambo kumi na tano ambayo kwa watu walio katika maisha ya ndoa wakiyazingatia kuna uwezekano mkubwa ndoa yao ikawa imara milele.

Ikumbukeni siku yenu ya ndoa
Inashangaza wanandoa kukumbuka siku zao za kuzaliwa na kuandaa sherehe lakini ni wachache sana wanaoikumbuka siku yao ya ndoa. Nishauri tu kwamba, siku yenu ya kuoana ni vyema mkaiweka kuwa miongoni mwa siku muhimu katika maisha yenu.
Mtakumbuka siku mliyoahidiana kuishi kwa shida na raha milele, mtakumbuka mlivyokuwa mnaahidiana kutokusalitiana. Nina imani ikiwa mnaikumbuka siku hii, kila mwaka mtakuwa ni kama mnafunga ndoa upya na hivyo inaweza kuifanya isichuje.

Heshimianeni
Kuolewa au kuoa ni heshima. Ni vyema wanandoa wakaheshimiana na katika siku zote za maisha yao kuhakikisha kila mmoja anakuwa muwazi na mkweli kwa mwenzake. Huu ni msingi madhubuti sana wa ndoa kwa sababu, kama mtakuwa mkidharauliana na kudanganyana, itaonekana hamheshimiani na hamko siriasi katika uhusiano wenu. Heshimianeni na ishini maisha yenu.
Vumilianeni
Mnatakikwa kufahamu kwamba, kila mmoja kakulia katika mazingira na malezi tofauti na mwenzake. Kwa maana hiyo, inawezekana mkawa mnatofautiana kitabia na mambo mengine. Kikubwa ni kuvumiliana! Mvumilie mwenzako kwa udhaifu aliokuwa nao na amini siku moja atabadilika.

Sameheaneni
Wanandoa ni watu ambao ni rahisi sana kukoseana mara kwa mara lakini dawa ya hali hii ni kila mmoja kuwa na moyo wa kusamehe na mwepesi wa kuomba msamaha pale anapomkosea mwenzake. Lugha ya upole ni vema ikatumika pale mmoja anapobaini amemkosea mwenza wake. Katika mazingira hayo ni wazi ndoa yenu haiwezi kuwa na nyufa.

Aminianeni
Yawezekana muda mwingi uko mbali na mwenzako wako kutokana na mihangaiko ya kimaisha. Mume/mkeo awapo mbali na wewe, amini kwamba yuko salama na hawezi kukusaliti. Ukishampenda na mkaingia kwenye maisha ya ndoa, amini kwamba ni wewe tu na mwingine hana nafasi katika ndoa yenu.Kwa kufanya hivyo penzi kati yenu litakuwa likiongezeka siku hadi siku.

Fundishaneni
Kama nilivyosema hapo juu, hakuna ambaye yuko kamili kwa maana hiyo ukigundua kuwa kuna baadhi ya maeneo mwenza wako hajakaa sawa, ni vizuri kumuelekeza. Fahamu kwamba mapenzi ya ndoa ni kama shamba, ni lazima lipaliliwe, lilimwe, liwekewe mbolea ili listawi. Hivyo basi, nawe katika kuhakikisha ndoa yako inakuwa na afya basi muelekeze mwenza wako pale anapotoka nje ya msitari.

Kila moja awe mfano
Waswahili wanasema kuwa, usimfanyie mwenzako kitu ambacho usingependa akufanyie. Hata katika maisha ya ndoa iko hivyo hivyo. Kwa mfano hutajisikia vizuri kama utabaini mumeo ana mtu mwingine nje ya ndoa, basi kuwa wa kwanza kuonesha mfano kwa kutulia katika ndoa yako.
Ni vizuri pia ukawa unamuonesha mwenza wako kwa mifano jinsi ambavyo ungependa awe au akufanyie. Si vizuri wewe uwe unataka ufanyiwe pasipo kuonesha njia. Unataka mawasiliano ya mara kwa mara, hivyo si vibaya ukaanza wewe kujenga utaratibu wa kumtwangia ili naye ajifunze na kufuata.

Kununuliana vijizawadi
Ukishaingia katika maisha ya ndoa suala la kumnunulia mpenzi wako zawadi linakuwa halina muda muafaka. Usisubiri kumnunulia mkeo au mume zawadi siku za sikukuu tu kana vile Valentines Day, Krismasi, siku za kuzaliwa na siku nyingine kama hizo.
umieni muda mzuri pamoja
Wapo ambao kwenda ‘out’ na wanandoa wenzao ni siku za sikukuu na yaweza kutokea hivyo mara moja kwa mwaka. Kitaalamu penzi la ndoa halijengwi kwa siku moja kama hivyo, inatakiwa mara kwa mara kuwa karibu na mpenzi wako muda unapopatikana.
Kama wewe ni mtu wa kuwa bize sana, fanya hivyo katika siku za wikiendi. Kaa na mwenza wako sehemu tulivu, badilishaneni mawazo, liwazaneni, zungumzieni maisha yenu ya baadaye. Naamini kwa kufanya hivyo huwezi kuyachukia maisha ya ndoa na unaweza kujikuta unanenepa kila siku.

Msigandane sana
Hapa namaanisha kwamba, licha ya kila mmoja kuwa na hamu kubwa ya kuwa karibu na mwenzake kila wakati lakini tujaribu kupunguza muda wa kuwa pamoja kwakuwa, huweza kuwasababishia mkachokana haraka.
Wapo baadhi ya wanawake ni ving’ang’anizi sana, mumewe akitoka kidogo kwenda kupiga stori na washkaji, tatizo! Akichelewa kidogo kurudi kazini, anamfuata huko huko au atamsumbua kwa simu kila wakati.
Vitu kama hivi vinaonesha namna mke alivyo na wivu lakini huu tunaweza kuuita wivu wa kijinga na unaweza kuwa kero kwa mwenzako. Niseme tu kwamba, kugandana sana kunawafanya mkinahiane mapema, hivyo peaneni uhuru katika maisha yenu, kikubwa ni kuaminiana.

Ridhishaneni
Maisha ya ndoa ni kuridhishana, katika hili najua mtakuwa mmeelekeza akili zenu katika suala zima la tendo la ndoa. Hilo nalo la msingi sana lakini pia ni lazima mridhishane katika mambo mengine yanayogusa moja kwa moja maisha yenu ya kila siku. Muulize mwenza wako nini angependa kukipata kutoka kwako, kama kiko ndani ya uwezo wako, mpatie na kile ambacho huwezi kumpatia, mpe sababu aridhike nazo.
Kwa kuridhishana, hakuna atakayekuwa na mawazo ya kutoka nje ya ndoa lakini kinyume chake utashangaa namna ndoa yenu itakavyokuwa inayeyuka taratibu mithili ya barafu lililotumbukizwa ndani ya maji ya moto.

Mfanye akuone ni wa pekee
Kama ni mwanaume umeoa, tambua huyo uliyemuoa wapo waliokuwa wakimpenda na kutamani kuwa naye pia. Mume unatakiwa kumfanya mkeo aamini kwamba, wewe ndiye uliyestahili kuwa naye na si wengine. Muoneshe upendo wa hali ya juu, mthamini, mheshimu na mjali. Ichote akili yake na umfanye aone bila wewe maisha yake hayajakamilika. Vivyo hivyo kwa mke.

Ombeni ushauri
Katika maisha yenu, mnaweza kujikuta mambo hayaendi kama vile mlivyokuwa mnatarajia. Wapo wazee mnaowaheshimu au wale wenye uzoefu wa muda mrefu katika maisha ya ndoa, waoneni waombeni ushauri katika mambo yanayowachanganya.

Mwenza wako kabadilika baa ya kuoana, jaribu kukaa naye mzungumze na ukiona hakuelewei, omba ushauri kwa watu wako wa karibu, usichanganyikiwe katika mambo ambayo unaweza kuyapatia ufumbuzi.
Hadi hapo naamini nitakuwa nimekupatia kile ambacho kinaweza kuleta mabadiliko katika maisha yako ya ndoa. Hadi wiki ijayo tena kwa mada nyingine kali zaidi. 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate