KLABU
ya Tottenham imefufua matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao
baada ya kuitandika mabao 3-1 Manchester City na kuwakatisha tamaa ya
kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kiungo
wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri aliifungia bao la kuongoza Man City
dakika ya tano, lakini baada ya hapo vijana wa Andre Villas-Boas
wakaigeuzia kibao City.
Kitu hicho: Gareth Bale akimtungua Joe Hart na kufanya 3-1
Clint Dempsey aliisawazishia Spurs dakika ya kabla ya 57 Jermain Defoe kufunga la pili dakika ya 79 na Gareth Bale kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City dakika ya 82.
Clint Dempsey aliisawazishia Spurs dakika ya kabla ya 57 Jermain Defoe kufunga la pili dakika ya 79 na Gareth Bale kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City dakika ya 82.
Matokeo hayo yanamaanisha Manchester
United wanaweza kujihakikishia ubingwa kesho wakishinda, kwani
watafikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.Kikosi
cha Tottenham Hotspur kilikuwa; Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen,
Assou-Ekotto, Sigurdsson/Holtby dk60, Dembele, Parker/Huddlestone dk61,
Bale, Dempsey na Adebayor/Defoe dk71.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy/Lescott dk90, Toure, Barry, Milner/Kolarov dk46, Tevez, Nasri na Dzeko/Sinclair dk82.
Shuti: Jermain Defoe akiifungia Tottenham bao la pili mbele ya Vincent Kompany
Ufufuko: Clint Dempsey akishangilia bao la kusawazisha aliloifungia Tottenham
Sita Bora ya Ligi Kuu England kabla ya matokeo ya Chelsea na Liverpool
No comments:
Post a Comment