EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, April 28, 2013

Watu 30 wavamia, kuvunja nyumba.

Dar es Salaam:
 Zaidi ya watu 30 usiku wa kuamkia jana walivamia na kuivunja nyumba ya Yasinta Malisa, iliyopo Kunduchi Ununio ,kando ya Bahari ya Hindi, huku wakimtishia kwa bastola mlinzi wa nyumba hiyo.

Kutokana tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amemtaka mmiliki wa nyumba hiyo kuwasilisha vielelezo vya umiliki wa eneo hilo polisi.
Hatua hiyo inalenga katika kuwawezesha polisi kuvipitia na kumpa ushauri wa ama kwenda mahakamani au kumkamata anayeshukiwa kubomoa nyumba hiyo.

“Wanatakiwa kuwasilisha vilelezo vya umiliki wa eneo hilo, lakini pia inaonyesha kuwa kuna mgogoro katika eneo husika. Vielelezo ndivyo vitaonyesha kila kitu na tutajua wapi kuna tatizo,” alisema Kenyela.


Mmoja wa walinzi wa nyumba hiyo, Saitoti Nang’oro na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ununio, Iddi Musa, walisema watu hao walivamia mtaa huo saa 9 usiku wakiwa na marungu, mapanga na bastola.
Akizungumzia na gazeti hili, Yasinta alisema baada ya kufiwa na mume wake mwaka jana, aliamua kuendeleza ujenzi wa nyumba hiyo, lakini siku tatu baada ya kuanza kazi, watu hao walivamia na kuivunja nyumba yake.

“Hili eneo tulilinunua kutoka kwa wazawa wa hapa Ununio na nina vilelezo halali, ila nashangaa kitendo kilichofanyika tena kimefanyika usiku, sasa kama wanamiliki eneo kihahali kwa nini waje usiku, mbona hakuna hata vilelelezo vyao katika ofisi za Serikali ya mtaa,” alihoji.
Alisema alinunua eneo hilo miaka 20 iliyopita, huku akisisitiza kuwa eneo hilo halijapimwa na Serikali na wamiliki wake wanauza maeneo yao kama mashamba. Akisimulia alivyonusurika kuuawa Nang’oro alisema akiwa lindoni, aliona kundi la watu likija na wakati akijiandaa kuwahoji walimkamata na kumfunga kamba.

“Mmoja ndio alinishika na kunifunga kamba, wengine walikuwa wakibomoa nyumba kwa kutumia vyuma vikubwa. Yule aliyekuwa amenishika alikuwa pia ameshikilia bastola na aliniambia kuwa nisipokuwa mtulivu au nikikimbia atanipiga risasi,” alisema Nang’oro.
Kwa upande wake, Musa alisema tangu achaguliwa kushika nafasi hiyo, vielelezo vilivyopo katika ofisi yake vinaonyesha kuwa mwenye eneo hilo ni Yasinta na siyo mtu mwingine.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate