JB akifungua Shampeni
Staa huyo wa filamu za Kibongo aliangusha bonge la sherehe kwenye Ukumbi wa Shekinah, Makonde, Mbezi Beach jijini Dar, Jumatano iliyopita na kuhudhuriwa na mastaa lukuki.

Uwoya Ndiku na Krrish Full Furaha
Krrish alikuwa akitimiza miaka miwili tangu alipozaliwa Mei 8, 2011 ambapo sherehe ilianza mchana hadi usiku mnene kukiwa na kila aina ya burudani hivyo kuwaacha watu midomo wazi kufuatia kufuru hiyo.
Uwoya,Ndiku wakikata Keki kwa pamoja na mtoto wao Krrish

MAAKULI MWANZO MWISHO
Kwa mujibu wa ‘balozi’ wetu, wageni waalikwa walipoanza kuingia ndani ya ukumbi, walikuwa wakikaribishwa kwa vinywaji vya kila aina na chakula kilichotengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu hata kabla pati hiyo haijaanza rasmi, zoezi ambalo liliendelea hadi mwisho.
Muonekano wa kekiKwa mujibu wa ‘balozi’ wetu, wageni waalikwa walipoanza kuingia ndani ya ukumbi, walikuwa wakikaribishwa kwa vinywaji vya kila aina na chakula kilichotengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu hata kabla pati hiyo haijaanza rasmi, zoezi ambalo liliendelea hadi mwisho.
WATOTO WATENGENEZEWA KAMA HOLLYWOOD
Katika shughuli hiyo, kulikuwa na michezo mbalimbali ya kisasa ya watoto walioalikwa ambao walijengewa vijumba ‘spesho’ vya kuchezea kama Hollywood, Marekani.
Shamsa Ford na Welu Sengo wakijiachia
ULINZI MKALI
Ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinachoweza kuleta ‘mizinguo’ na kuhatarisha burudani, kulikuwa na mabaunsa wapatao saba waliokuwa wameweka ulinzi mkali.
UWOYA, NDIKU
Huku watu wakiendelea kugonga ‘mpunga’, vinywaji na muziki, waliingia wazazi wa Krrish, Uwoya akifuatana na Ndiku wakiwa wamembeba mtoto wao na kusababisha shangwe za makofi na vigelegele.
MAPENZI MOTOMOTO
Uwoya na Ndiku, muda wote walionekana wakiwa katika mapenzi motomoto kwa kukimbizana ukumbini kwa mabusu ya kumwaga.
BONGO MOVIES
Katika mnuso huo, mastaa mbalimbali kutoka Bongo Movies walipoingia ukumbini walichangamsha sherehe kwani mara zote walikuwa wakifurahi na kuserebuka muziki.
JB AFUNGUA SHAMPENI
Kulikuwa na shampeni zipatazo arobaini ndani ya ukumbi huo lakini Steven Jacob ‘JB’ aliombwa kufungua moja kwa ajili ya kuziwakilisha nyingine huku watu wakimuimba; ‘Bonge la Bwana’ na kumfanya kuona soo kimtindo.
BIBI, BABU KRRISH
Chereko zilikolea baada ya baba na mama mzazi wa Uwoya, kujichanganya na wageni waalikwa huku wakicheza na kufurahi kwa pamoja.
WATOTO YATIMA
Ili kuonesha anajali watoto wengine ambao wazazi wao wametangulia mbele ya haki, staa huyo aliwaalika watoto yatima ili kusherekea na Krrish siku hiyo.
Hadi Risasi Jumamosi linaanua jamvi ukumbini hapo usiku, watu walikuwa wakiendelea kutandika ‘masanga’ na kuserebuka muziki.

CHANZO NI GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment