EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, May 10, 2013

KIOJA 2013 MWANAUME KWA MWANAUME WAFUMANIWA LAIVU GESTI.

MWANAUME aliyefahamika kwa jina la baba Salome, mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alimdhalilisha mkewe (mama Salome) baada ya kufumaniwa gesti akiwa na mwanaume mwenzake ambapo madai yalisema, walikuwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili.
Habari na Global Publishers.


Baba Salome (kulia) na Julius Mwita baada ya kufumaniwa wakiwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili.
Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.
HABARI ZA AWALI
Awali ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia kwenye gesti moja ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa wakiwafahamu.
Mama Salome akimpa kisago mumewe baada yakumfumania akiwa na Mwita (kushoto) anayedaiwa kuwa shoga.
“Unajua tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume mwenzake walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia nyingine pia wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni wawili hao kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja.
Akaendelea: Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, baba Salome ni mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema ana ‘katabia’ ka kutaka kuwa faragha na  wanaume wenzake bila kujulikana nini anakitaka katika usiri huo.

...Songombingo likiendelea ndani ya gesti.
Madai zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda kwenye gesti walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa wanakitaka, ndipo siri ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba cha kupumzika kwa siku hiyo lakini kwa sheria za Jiji la Dar es Salaam (kama siyo za nchi nzima), wanaume wawili hawaruhusiwi kulala chumba kimoja.
Chanzo kikasema: Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya tukio, wakapewa chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa baba Salome na kumtonya mkewe, mama Salome kwamba mumewe ameingia gesti.
MAMA SALOME AJA JUU, AMTAJA KIDAWA
Kichekesho zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa mumewe amezama gesti, mama Salome ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika kutoka  kwenye mikopo ya Finca, alitoka mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la kulia Kidawa akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo.
Umati ukiwashangaa wanaume hao waliofumaniwa gesti.
“Watu walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa bali mwanaume mwenzake. Kwanza mama Salome aliomba asitaniwe juu ya hilo, lakini akasisitiziwa,” alisema mtoa habari huyo.
NJE YA GESTI, MAMA SALOME AFUNGUKA
Akizungumza kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, mama Salome alisema kwamba alipata taarifa siku nyingi mumewe ana ukaribu na mwanaume huyo ambaye mitaani watu wanasema  anajihusisha na vitendo vya ushoga.
“Nilipozipata taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti na mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema mwanamke huyo kisha akazama ndani ya gesti akiwa na polisi ambao haikujulikana walikotokea.
...Bwana Mwita akijaribu kukimbia songombingo hilo.
FUMANIZI TAAP!
Huku mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili wala lile kule chumbani, mlango ulisukumwa na kufunguka ambapo mwanamke huyo aliwakuta wawili hao wakiwa wameshavua baadhi ya nguo. Wote walishtuka kuona wameingiliwa!
“Yaani roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa kwangu mpaka unakuja kwa mwanaume mwenzako jamani baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome.
MWANAUME MMOJA AANGUA KILIO
Baada ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na baba Salome aliangua kilio huku  akiomba kusamehewa kwa vile yeye ni mume wa mtu, lakini kilio chake hakikusikika kwa polisi ambapo waliwafunga pingu na kuwataka kuelekea katika kituo cha polisi.
...Watuhumiwa wakipelekwa kituo cha polisi.
MMOJA ALIA NA MAPAPARAZI
Wakati wakitoa maelezo kwenye kituo cha polisi, mwanaume aliyekuwa na baba Salome alijitambulisha kwa jina la  Julius Mwita, mkazi wa Devi’s Corner ana  mke na watoto wawili na aliwaomba sana mapaparazi wamhifadhi kwani wakwe zake wakimuona ‘itakula  kwake’.
“Jamani mapaparazi nipo tayari kwa lolote naomba sana tuyamalize hapahapa, mimi ni mume wa mtu, wakwe zangu wananiheshimu na kunithamini sana,” alisema Mwita.  
Hata hivyo, pamoja na kilio hicho mwanaume huyo aliishia kuswekwa lupango na baadaye kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kwa hatua zaidi.
Imeandikwa na Issa Mnally, Gladness Mallya, Issakwisa Mponi, Makongoro Oging na Imelda Mtema.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate