EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, May 15, 2013

Ngassa asaini Yanga miaka 2 atakuwa analipwa dola 2000 (Sh milioni 3.2) kwa mwezi.

KIUNGO mwenye kasi, Mrisho Khalfan Ngassa, amerejea Yanga na kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea tena timu hiyo.
Ngassa alianza kupata umaarufu mkubwa akiwa na Yanga kabla ya kuondoka na kujiunga na Azam FC kwa kitita cha jumla ya Sh milioni 98 na kuweka rekodi mpya ya usajili.
Mrisho Khalfan Ngassa.
Lakini Ngassa ameamua kusaini tena mkataba wake mpya Yanga wakati akiwa chini ya klabu ya Simba ambao ni watani wakubwa wa Yanga.
 
Simba na Yanga zinakutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho kufunga msimu, huku Yanga wakiwa wamepania kulipa kisasi cha mabao 5-0.
Mechi hiyo ndiyo itakuwa ya mwisho kwa Ngassa ambaye mkataba wake umesainiwa bila kuwa na tarehe, Championi Jumatano limeshuhudia na lina uhakika asilimia mia.

“Mkataba na Ngassa kila kitu kimekamilika kama unavyoona, hapa tunachosubiri ni kuisha kwa msimu na mara moja atatua na kuanza kazi Jangwani,” alisema mmoja wa viongozi ambao huhusika na masuala ya usajili Yanga.
Alipoulizwa kwa nini mkataba huo ambao una saini ya Ngassa na dole gumba lake hauna tarehe, alijibu:
 
“Bado hatujajua utaratibu wa TFF kama mkataba ukisainiwa kabla ya mwingine kuisha inakuwaje. Hatutaki kuingia kwenye matatizo na mtu.
“Kitu kizuri Ngassa baada ya mkataba wake na Azam FC kuisha, sasa ameamua kurudi nyumbani, nasi tumemkaribisha vizuri.”
Ingawa mhusika alifanya juhudi za kuficha eneo la malipo ya Ngassa lakini taarifa za uhakika zinaonyesha atakuwa analipwa dola 2000 (Sh milioni 3.2) kwa mwezi.
 
Kwa mshahara, Ngassa atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi ya wachezaji wote Ligi Kuu Bara. Labda kama kuna timu kati ya Yanga, Simba au Azam FC itasajili mwingine na kumpa zaidi ya hizo.
Kwa misimu miwili Felix Sunzu amekuwa akiongoza. Analipwa dola 3,500 (Sh milioni 5.6), 

Mzambia huyo amemaliza mkataba na Simba, ataondoka. Wakati Ngassa akiwa Azam na Simba alikuwa anachukua Sh milioni 2 kwa mwezi.
 
Kuhusiana na fedha za usajili, kwa kuwa Ngassa ametua Yanga kama mchezaji huru, tayari ameshatanguliziwa ‘kishika uchumba’ cha Sh milioni 10 pamoja na gari aina ya Nissan Trail ambalo thamani yake inafikia hadi Sh milioni 23.
 
Ngassa amekuwa akilitumia gari hilo alilopewa na Yanga baada ya kuuza alilopewa na Simba aina ya Toyota Verrosa lenye thamani ya Sh milioni 16 kwa hofu ya kupokonywa na Simba siku atakaposema anakwenda Yanga.
Kuna taarifa kuwa Ngassa alisaini mkataba mwingine na Simba ambao angeanza kuutumikia baada ya mechi hiyo ya Jumamosi.
 
Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope, imetangaza kwamba Ngassa alisaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja, akapewa gari na fedha Sh milioni 30 na kama anataka kwenda kokote, basi atalazimika kurudisha fedha hizo.
Lakini Ngassa amekuwa akisisitiza hana mkataba na Simba na baada ya huo wa Azam FC iliyompeleka Simba kwa mkopo utakapomalizika, atakuwa huru kwenda anakotaka.
Ngassa ambaye yuko kambini na Simba mjini Zanzibar, amewahi kuliambia Championi kwamba kama Simba inamtaka abaki, basi lazima itoe kitita cha Sh milioni 150.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate