Clara amemfungulia MARA na kutoroka, lakini Gary anafika na
na kumuuliza Clara kwanini amemfungulia MARA? Lakini akiwa bado ameshikilia
bastola na hasila za kufa mtu, polisi wanafika.
Gary anafanikiwa kukimbia
na kuruka ndani yam to na kuwachenga polisi. Tayari Clara ameanza
kumsaliti baba yake “Gary” kwa kumfungulia MARA. Lakini pia Clara huyo huyo
anamsaliti Gary baada ya Gary kumpigia simu huko alikofanikiwa kutorokea
akimtaka Clara aongozane nae ili wakapande boti watoroke kusikojulikana.
Lakini Clara anaanza kukumbuka usemi wa MARA aliomwambia
kipindi cha nyuma kuwa “Gary anataka tu akutumie kama chambo ili ampate mama (Alvira)”.
Baada ya Clara kuwaza hivyo, anaamua kwenda hadi kwa akina MARA na kuanza
kutubu mbele ya MARA huku akijutia yote aliyomfanyia tokea mwanzo.
Baada ya Gary kugundua kuwa Clara amemsaliti kwa kwenda
kuwaambia akina AMANTE mpango wa Gary kutaka kutoroka naye, sasa Gary anaamua kumpigia
simu Clara na kumpa vitisho “kwakuwa umeamua kunisaliti , wakati wewe ndiye
niliyekuwa nibebakia na wewe, upendo wangu woote nilikupatia, sasa maisha yako
yote yatakuwa ya shida” alisema Gary.
Usiku Alvira akiwa kwake kupitia dirisha lake anamuona mtu
akinyemerea nje ya nyumba yao, Alvira anamuita mumewe “Amante” kwa sauti kubwa “Amante!!
Amanteee!! Namante anawapigia polisi simu. Polisi wanafanikiwa kumkamata mtu
huyo, lakini mtu huyo alikutwa na kibox kidogo na alisema kuwa kunamtu
alimuagiza akifikishe kwa Alvira.
Ndani ya kibox kulikuwa na bonge la pete pamoja na Ujumbe wa
malavidavi ambao kumbe Gary ndiye aliyeuandika ili umfikie kipenzi chake
Alvira. Alvira anausoma na kujikuta akimuuliza mumewake Ujumbe huu unamaana
gani!?.
Baada ya kuona kasha kasha za Gary zinazidi kuchukua sura
mpya, Alvira na Amante wanaamua kumchukua MARA na SUZAN na kuwakodishia gari
ili iwatoroshe kuwaokoa na balaa za Gary. Wanapanda gari, wakiwa safarini
wanasinzia wote wakimuacha dereva akiendesha. Mara ghafla mbele ya safari, Gary
anaonekana ndiye dereva wa lile gari, ile MARA na Suzan wanashtuka kuuliza
dereva, Gary anashuka na kuwafungulia mlango, wanapigwa na butwaa!!!.
Gary anawateka na bastora na kuwaamuru waingie katika jengo moja
linalotisha kinyama, Gary anaamua kumwambia MARA kuwa yeye ndiye chanzo cha
maisha yake kuharibika nayeye ndiye aliyesababisha mdogo wake Cairlo afariki dunia, na tokea
MARA akizaliwa alikuwa kikwazo ndio maana akafanya mipango wakabadilishwa na
Clara ili Clara apate maisha mazuri.
Wakati huo Suzan ni mja mzito lakini Gary anamsukuma hadi
chini wakiwa na MARA, baada ya unyama wa Gary kuzidi MARA anamwambia Gary “yani
huna hata huruma kwa mwanao aliyeko tumbini? Gary anamfuata Suzan kwa upole na
kumwambia kuwa unamtoto tena? Mimi
ninaye mtaka ni Alvira na Clara tuu!
Gary anamchukua MARA na kumfungia ndani ya Tanki la maji na
kufungulia maji huku akirudishia mfuniko. Maji yanazidi kujaa, wakati gary
akiwa nje Amante, Alvira na Clara wanawasili huku Amante akiwa ameshikilia
bastola. Mpango ulikuwa hivi, Gary alimtaka Clara aletwe ili wabadilishane na
MARA.
Walipofika Gary anamuamuru Amante aweke basola chini ili
kumnusuru mwanae MARA.Amante mara baada ya kuiweka chini Gary anaishika na
kumkabidhi Alvira na kumuambia bila kupoteza muda muuwe mumeo ili umuokoe MARA,
ukishindwa atakufa. Alvira anachukua bastora na kumnyooshea Gary. Gary na kumuambia
“ ukiniripua utamkosa MARA”. Alvira naamua kijinyooshea bastola yeye mwenyewe
ili ajiuwe, lakini Gary anamshika mkono na kuanza kujibizana, lakini ile Gary amegeuka,
Amante alijaribu kumpora bastola.
Wakati seke seke likiendelea, huko MARA maji tayari
yamekwisha mfunika hadi juu ya kichwa, lakini Clara nafanikiwa kwenda kumtafuta
MARA. Anafika alikofungiwa MARA,anaona chini cheni ya shingoni ya MARA ikiwa
nchini, anapata wazo la kufunua tanki la maji na kumkuta MARA ndani yake,
anamuokoa.
Amante anaikosa bastola na Gary kufanikiwa kumtupa chini ya
ghorofa hilo. Gary anamrudia Alvira lakini
anakosea na kumshuti mwanae CLARA hadi chini. Ile anataka kumshuti Alvira,
Suzan anatoka kwa nyuma akiwa amebeba
bonge la chuma na kumtandika kichwani, ile bado anataka kumshuti Alvira, SUZAN
anamchoma GARY chuma tumboni na kumuua, lakini kabla hajafa alifanikiwa
kumuambia mama yake kuwa “mama nakupenda, nakumpenda sana” baada ya maneno hayo
alikata roho. Siku iliyofuata SUZAN alijifungua watoto mapacha na wote
walioigiza Tamthilia ya MARA CLARA walionekana wote kwa pamoja wakipata picha
ya ukumbusho, isipokuwa Gary hakuwepo.
Niwashukuru wapenzi woote wa “TAMTHILIA YA MARA CLARA” kwa
kutenga muda wenu na kutembelea blog yetu ya “ASILI YETU TANZANIA”. Pia
niwashukuru kwa dhati kituo cha Luninga cha STAR TV kwa kuonyesha Tamthilia
nzuri na iliyovutia watu wengi. Pia niwashukuru tovuti na blog mbali mbali
waliokuwa wakishare story hii katika site zao. Naomba mniadd kwenye site zenu.
------------------------MWISHO WA TAMTHILIA YA “MARA
CLARA”-------------------------------
No comments:
Post a Comment