Bahi.
Mbunge wa Bahi, Omar Badwel (CCM) amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi wa Kijiji cha Bahi Makulu, wilayani hapa kumtaka awaeleze sababu za kutoa ahadi ya uwongo kuwajengea bwawa la maji ambayo hajaitekeleza.
Mbunge wa Bahi, Omar Badwel (CCM) amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi wa Kijiji cha Bahi Makulu, wilayani hapa kumtaka awaeleze sababu za kutoa ahadi ya uwongo kuwajengea bwawa la maji ambayo hajaitekeleza.
Badwel alikutana na mkasa huo juzi alipoongozana na viongozi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, kwenda kijijini hapo kukutana na wananchi waliodai kuathirika na madini ya Urani.
Wananchi hao walimtaka mbunge huyo kuwaeleza sababu za kutotimiza ahadi yake ya kuwajengea bwawa la maji, aliloahidi kwenye kampeni wakati akigombea mwaka 2010.
Akijitetea mbele ya wananchi, Badwel alikiri kuwa
hajatekeleza ahadi hiyo, hali iliyomfanya asiwe na ujasiri wa kuhudhuria
mkutano huo kwa kuogopa kuulizwa maswali yanayohusiana na bwawa hilo.
“Ni kweli naikumbuka ahadi yangu ya kuwajengea bwawa ambayo sijaitimiza hadi leo. Ndiyo maana mkuu wa wilaya aliponiambia ninatakiwa kuja huku nilitaka kukataa kwa kuhofia maswali kuhusu ujenzi wa bwawa hili,” alisema Badwel.
Hata hivyo, Badwel alisema fedha za kujengea bwawa
hilo ambalo litagharimu Sh80 milioni, zimepatikana ingawa siyo zote
kwani ni Sh42 milioni zilizopo kiwango ambacho hakitoshi kukamilisha
ujenzi huo.
Wakizungumza kwenye mkutano huo, wananchi walionekana kuchoshwa na ahadi hewa na kumweleza mbunge huyo kuwa, kama asipojenga bwawa hilo kwa wakati basi atambue hatapata kura zao mwaka 2015.
Badwel aliwaomba wananchi kumvumilia kwa kipindi hiki kifupi, ili ajitahidi kutafuta fedha za kukamilisha ujenzi wa bwawa hilo ambalo ni tegemeo kwa wanakijiji hao.
“Hivi kama niliahidi vitu 15 na nimetekeleza vitu
12 na kuacha vitu vitatu, mnataka kunihukumu kwa kutotekeleza hayo mambo
matatu na kuyaacha mengi mazuri niyofanya? Msifanye hivyo ndugu zangu
kila nililoahidi lazima nitatekeleza hata kama kwa kuchelewa,” alisema
Badwel.
No comments:
Post a Comment