Dar es Salaam.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imewapiga marufuku
wafanyabiashara wa dawa na vipodozi wanaouza kwenye vyombo vya usafiri
na kuwataka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Wananchi
pia wametakiwa kuacha kununua bidhaa hizo kwenye vyombo vya usafiri
kutokana na ubora na usalama wake kuwa wa shaka na matumizi yake ni
hatari kwa afya.
Katika taarifa iliyotolewa na TFDA kwenye vyombo vya
habari jana, ilieleza kuwa kumekuwa na tabia ya wafanyabiashara wadogo
kuuza bidhaa aina ya dawa katika vyombo vya usafiri hasa treni na mabasi
ya abiria ambapo ni kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
inaeleza kuwa dawa na vipodozi ni bidhaa zinazotengenezwa na kemikali
zenye sumu zinazodhibitiwa na TFDA ambapo baadhi ya bidhaa zinatakiwa
ziuzwe na kuhifadhiwa katika maeneo ambayo yanakidhi matakwa ya uhifadhi
na uuzaji.
Ilieleza kuwa bidhaa hizo zikihifadhiwa katika maeneo
yenye joto jingi, pachafu na pasipo na uangalizi wowote zinakuwa duni,
kushindwa kutibu na kutengeneza sumu zinazoweza kumwathiri m tumiaji.
No comments:
Post a Comment