Ndege aina ya bundi na wanyama kama nyoka na nyani ni miongoni
mwa bidhaa ambazo zimekuwa zikiingizwa nchini na kusamehewa kiasi
kikubwa cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), karibu kila mwaka.
Bidhaa nyingine ambazo pia zilipewa msamaha kati ya mwaka 2003 na mwaka 2008 ni mayai ya ndege mabichi, yaliyopikwa, yaliyochemshwa, yaliyomenywa kiasi cha tani 1,423.3 na msamaha wake wa kodi ulikaribia Sh398 milioni.
Misamaha ya kodi ni moja ya mambo yanayotarajiwa kutawala mjadala wa bajeti kuu ya Serikali ya 2013/14 ambao unatarajiwa kuanza kesho mjini Dodoma huku kukiwa na malalamiko mengi yanayokosoa bajeti hiyo iliyowasilishwa bungeni Alhamisi wiki hii na
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
Katika hotuba yake Dk Mgimwa alisema atapendekeza
marekesbisho ya Sheria ya VAT ili kupunguza misamaha ya kodi, ijapokuwa
hakuweka bayana ni kiasi gani misamaha hiyo itapunguzwa.
Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haujawa tayari kutoa ufafanuzi kuhusu misamaha hii ya kodi ambayo inatolewa kwenye bidhaa ambazo zinapatikana kwa wingi kwa maelezo kwamba ulikuwa bado unalifanyika kazi suala hilo.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa
bidhaa ambazo zimekuwa zikipewa misamaha hiyo ya kodi, nyingi zinauzwa
kwenye maduka makubwa (Super markets) kwa bei ya chini, hivyo kuziweka
njiapanda bidhaa kama hizo zinazozalishwa hapa nchini. Kwa upande wa
wanyama na ndege wanaoingizwa nchini na kusamehewa kodi, wengi wanafugwa
katika makazi ya watu wakiwamo raia wa kigeni na Watanzania.
Uchambuzi uliofanywa na gazeti hili katika takwimu za misamaha ya kodi unathibisha kuwa miaka ya 2003, 2004 na 2007, ndege 147, 091 mchanganyiko wa bundi na kasuku waliingizwa nchini na kusamehewa kodi inayofikia Sh98.2 milioni.
Hesabu hiyo ni jumla ya bundi, kasuku na ndege wengine 146,607 walioingizwa nchini 2003 na 2004 kusamehewa VAT Sh90.6 milioni wakati 2007 bundi 484 walioingizwa nchini walipata msamaha wa Sh7.6 milioni.
Taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo gazeti hili limeziona zinathibitisha kwamba nyani 29,829 waliingizwa nchini mfululizo kuanzia 2005 hadi 2008 na kodi iliyosamehewa karibu Sh5 milioni.
Mwaka 2007 ndiyo unaongoza kwa kuingiza nyani wengi kutoka nje ya nchi ambao wanafikia 27,992, hivyo kusamahewa Sh4,095,481. Miaka mingine ni mwaka 2005 ambapo nyani 463 walisamehewa Sh60,523, mwaka 2006 ambao uliingiza nchini nyani 1,169 waliosamehewa Sh522,425, wakati 2008 nyani 25,744 walisamehewa kodi ya Sh283,328.
Orodha ya bidhaa hizo inaonyesha kuwa mwaka 2007
waliingizwa nchini nyoka 31 ambao walipewa msahama wa kodi wa
Sh2,098,430 na mwaka huohuo waliingizwa nchini nyangumi 149 ambao
walisamhemewa kodi ya Vat Sh25,744.
Miaka mingine ni 2003 mbwa na paka 14,693 waliosamehewa Sh9,267,063, mwaka 2004 idadi yao ilikuwa 2,203 msamaha wa Sh2,672,379, mwaka 2005 walikuwa 2,384 na kusamehewa 4,355,684, mwaka 2006 idadi ilikuwa 5,373 na walisamehewa Sh2,712,650 na 2008 idadi yao ilikuwa 7,076 na msamaha ni Sh18,220,333.
Kwa upande wa mayai ya ndege; mabichi, yaliyopikwa, yaliochemshwa na yaliyomenywa, mwaka 2003 ziliingizwa tani za mayai ya ndege, yalio mabichi, yaliyopikwa, yaliochemshwa, yaliyomenywa tani 312.685 na kusamehewa kodi ya Sh147,269,138, mwaka 2004 tani 155.572 na kusamehewa Sh65,279,930.
Mwaka 2005 tani 16.744 za mayai zilisamehewa Sh13,951,583, mwaka 2006 tani 138.458 na kusamehwa Sh36,686,219, mwaka 2007 ziliingizwa tani 361.963 ambazo zilisamhemewa kodi ya Sh90,980,129 na mwaka 2008 ziliingizwa tani 125.252na kupewa msamaha wa Sh43,340,367.
Bidhaa nyingine ambazo zilisamehewa kodi ni tani 143.5 za mahindi mabichi ya kuchoma na kuchemsha ambayo yaliikosesha Serikali kiasi cha Sh15.8 milioni pamoja na tani 7.982 za miwa ambazo zilisamehewa kodi inayofikia Sh9.7 milioni.
Orodha ya bidhaa ambazo zimekuwa zikipewa msamaha wa kodi ya VAT pia zinajumuisha ndimu na malimao kiasi cha tani 171 ambazo zililikosesha taifa kiasi cha Sh10.7 milioni katika miaka hiyo sita.
Wanyama wengine
Mbwa na paka ni miongoni mwa wanyama ambao kati ya
mwaka 2003 na 2008 walisamehewa kodi ya VAT inayofikia 86,938,064,
wakiwa kwenye kundi la wanyama 73,804. Mwaka unaoongoza kwa kuingiza
mbwa na paka wengi ni 2007 ambapo idadi ya walioingizwa ni 42,175 na
kusamehewa kiasi cha Sh49,709,955.
Miaka mingine ni 2003 mbwa na paka 14,693 waliosamehewa Sh9,267,063, mwaka 2004 idadi yao ilikuwa 2,203 msamaha wa Sh2,672,379, mwaka 2005 walikuwa 2,384 na kusamehewa 4,355,684, mwaka 2006 idadi ilikuwa 5,373 na walisamehewa Sh2,712,650 na 2008 idadi yao ilikuwa 7,076 na msamaha ni Sh18,220,333.
Kwa upande wa mayai ya ndege; mabichi, yaliyopikwa, yaliochemshwa na yaliyomenywa, mwaka 2003 ziliingizwa tani za mayai ya ndege, yalio mabichi, yaliyopikwa, yaliochemshwa, yaliyomenywa tani 312.685 na kusamehewa kodi ya Sh147,269,138, mwaka 2004 tani 155.572 na kusamehewa Sh65,279,930.
Mwaka 2005 tani 16.744 za mayai zilisamehewa Sh13,951,583, mwaka 2006 tani 138.458 na kusamehwa Sh36,686,219, mwaka 2007 ziliingizwa tani 361.963 ambazo zilisamhemewa kodi ya Sh90,980,129 na mwaka 2008 ziliingizwa tani 125.252na kupewa msamaha wa Sh43,340,367.
Bidhaa nyingine ambazo zilisamehewa kodi ni tani 143.5 za mahindi mabichi ya kuchoma na kuchemsha ambayo yaliikosesha Serikali kiasi cha Sh15.8 milioni pamoja na tani 7.982 za miwa ambazo zilisamehewa kodi inayofikia Sh9.7 milioni.
Orodha ya bidhaa ambazo zimekuwa zikipewa msamaha wa kodi ya VAT pia zinajumuisha ndimu na malimao kiasi cha tani 171 ambazo zililikosesha taifa kiasi cha Sh10.7 milioni katika miaka hiyo sita.
Mwaka 2003 ziliingizwa tani za malimao 18.845 na
kusamehewa Sh3,971,367, mwaka 2004 tani 16.275 zilizosamehewa
Sh2,023,994, mwaka 2005 tani 1.375 zilizopewa msamaha wa Sh367,352,
mwaka 2006 tani 15.235 zilizosamehewa Sh2,339,456, mwaka 2007 tani 3.375
zilisamehewa Sh830,467 na mwaka 2008 tani 115.580 zilisamehewa
Sh1,163,779.
No comments:
Post a Comment