Chamwino.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, Fatuma Ali amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa kwa wakulima wilayani kwake.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, Fatuma Ali amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa kwa wakulima wilayani kwake.
Akizungumza ofisini kwake hivi karibuni, Ali alisema wakulima wamehamasika lakini mabadiliko ya tabianchi yanakwamisha jitihada zao.
“Tuna matatizo ya kupata mvua zisizokuwa kwenye mtiririko mzuri, mwaka huu kilichotokea wale waliopanda kwa mvua za mwanzo mazao yao yamekauka, waliovuna ni wale waliopanda mara mbili au tatu,” alisema Ali.
Ali alisema waliojiunga kwenye vikundi kwa ajili ya kilimohai wamevuna tofauti na wengine, lakini kinakumbwa na changamoto ya kushirikina.
“Mwingine anajifunza kwa mwenzake lakini wengine
wana imani za kishirikiana, hao ndiyo tunajaribu kuwaelimisha,” alisema.
Kuhusu vocha za pembejeo za ruzuku, Ali alisema wamepata kwa mara ya
kwanza mwaka huu na waliofungua milango ni Shirika la Chakula Duniani
(Fao), waliochagua baadhi ya vijiji walivyoona ni maskini zaidi.
Alisema Fao ilifuatiwa na Shirika la Toam kwa kushirikiana na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), wanaojihusisha na kilimo hao.
Ofisa Uraghibishi na Mawasiliano wa TFCG, Jacquiline Tesha alisema bila kushirikisha wakulima kutumia kilimohai, hawawezi kufikia malengo yao.
ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Alisema lazima mbinu mbalimbali zikusanywe kufikia malengo hayo.
No comments:
Post a Comment