UHAKIKI WA WASTAAFU NA WATEGEMEZI
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawakumbusha wastaafu na wategemezi wanaolipwa pensheni na Mfuko huu kufika na kujihakiki katika Ofisi za PSPF zilizopo katika Makao Makuu ya Mkoa uliopo. Mstaafu au mtegemezi anatakiwa kujihakiki kila baada ya miezi sita yaani Januari na Julai.
Fika kujihakiki ukiwa na nyaraka zifuatazo:
Wastaafu na Wategemezi waliopo Zanzibar watahakikiwa tarehe 1-3 Julai 2013 Makao Makuu ya Polisi (Ziwani) Unguja na tarehe 4-5 Julai 2013 ofisi za Polisi Chake Pemba. Kutojihakiki kwa muda unaotakiwa kutasababisha malipo yako ya pensheni kusitishwa bila taarifa.
“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma

- Kitambulisho cha mstaafu au mtegemezi au kadi ya mpiga kura (endapo hujapatiwa kitambulisho),
- Kadi ya benki unayopokelea pensheni,
- Picha moja ndogo ya rangi (passport size)
Wastaafu na Wategemezi waliopo Zanzibar watahakikiwa tarehe 1-3 Julai 2013 Makao Makuu ya Polisi (Ziwani) Unguja na tarehe 4-5 Julai 2013 ofisi za Polisi Chake Pemba. Kutojihakiki kwa muda unaotakiwa kutasababisha malipo yako ya pensheni kusitishwa bila taarifa.
“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
No comments:
Post a Comment