TUMSHUKURU Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku hii. Hakika Mungu ni mwema na anatupenda sana ndiyo maana tupo hapa leo.
Ndugu zangu, leo nitaizungumzia Bajeti ya Serikali ya Tanzania ambayo iliwasilishwa Bungeni wiki iliyopita ikieleza mapendekezo yake kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2013/14.
Ndugu zangu, leo nitaizungumzia Bajeti ya Serikali ya Tanzania ambayo iliwasilishwa Bungeni wiki iliyopita ikieleza mapendekezo yake kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2013/14.
Katika
mapendekezo hayo, serikali imepanga kutumia Shilingi trilioni
18,248,983 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Kwa tafsiri
yoyote ile, bajeti hiyo inaonyesha bayana kwamba siyo endelevu, kwani
kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 12,575 zitakuwa za matumizi ya
kawaida wakati Shilingi trilioni 5,674 tu ndizo zitatumika katika
miradi ya maendeleo.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa alisema matumizi hayo ya kawaida yanajumuisha shughuli zisizo za uzalishaji, zikiwamo mishahara ya watumishi wa serikali, taasisi na wakala za serikali, mfuko mkuu wa serikali na kile kinachoitwa “Matumizi Mengineyo” ya Shilingi 4.5 trilioni.

Kifupi tunaweza kusema hii ni
bajeti ya matumizi na siyo ya maendeleo na haionyeshi dhamira ya
serikali ya kumkwamua mwananchi wa kawaida kutoka katika dimbwi la
umaskini.
Matarajio makubwa ya Watanzania waliokuwa wakifuatilia hotuba hiyo ya waziri wa fedha yalikuwa kuona bajeti ya kuwaletea unafuu katika maisha yao ya kila siku, bajeti yenye mwelekeo wa kuwapunguzia umaskini na kukuza hali ya kiuchumi kwa mtu mmojammoja, makundi mbalimbali na taifa kwa jumla.

Tulio wengi tulitegemea
bajeti hiyo ilenge katika kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa
ajili ya maendeleo endelevu kupitia mfumo mpya uliowekwa na serikali wa
utekelezaji wa miradi ya kipaumbele inayotegemewa kuleta matokeo makubwa
kwa haraka.
Matumaini hayo makubwa yalitokana na ukweli kwamba bajeti hiyo iliyowasilishwa Bungeni ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Miaka Mitano ambao umeweka kipaumbele katika maeneo makuu sita ambayo ni maji, nishati, elimu, uchukuzi, kilimo na kuongeza mapato.

Hata hivyo, bajeti hiyo haionyeshi kuweka
mkazo katika utekelezaji wa vipaumbele hivyo kwa vitendo wakati imetenga
zaidi ya asilimia 60 kwa matumizi ya kawaida, huku miradi ya maendeleo
kama barabara ikipewa fedha kidogo tu.
Hotuba ya bajeti hiyo kwa kiasi kikubwa imejaa siasa na maelezo matamu ya jumlajumla tu. Uchambuzi wa haraka wa hotuba za bajeti za miaka ya hivi karibuni unaonyesha kwamba hiyo iliyosomwa wiki iliyopita haitofautiani sana na hizo zilizopita isipokuwa katika maeneo machache sana.

Kwa kutoa mfano,
serikali inasema bajeti ya mwaka 2013/14 ina shabaha na malengo ya
uchumi manane, ikiwa ni pamoja na kuwa na akiba ya fedha za kigeni
zitakazokidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje, lakini haisemi
lolote kuhusu mkakati wa kupata fedha zaidi za kigeni kutokana na
kuongeza kwa uzalishaji wa bidhaa zetu nje kwa lengo la kuweka
ulinganifu wa kibiashara.
Serikali pia imetamka kuwa ina shabaha ya
kupunguza mfumuko wa bei hadi digitali moja ajabu ni kwamba haijasemi
itatumia mkakati gani wakati mwaka uliopita mfumuko wa bei uliongezeka
kwa asilimia 16 kutoka asilimia 12.7 mwaka 2011.
Bajeti hii
inaendeleza utamaduni wa kupandisha kodi katika maeneo yaleyale
tuliyoyazoea kama kwenye bia, sigara, vinywaji baridi, leseni za magari,
mafuta na kadhalika. Inajulikana wazi kwamba kupanda bei ya mafuta,
kutapandisha bei za vyakula na gharama za huduma mbalimbali.
Waziri
Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itapandisha ushuru
wa mafuta ya dizeli kutoka Shilingi 215 kwa lita hadi Shilingi 217 kwa
lita, likiwa ni ongezeko la shilingi 2, mafuta ya petroli kutoka
Shilingi 339 kwa lita hadi Shilingi 400, ongezeko la shilingi 61 na
ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka Shilingi 200 kwa lita hadi shilingi
263 kwa lita, sawa na ongezeko la Shilingi 63 kwa lita na wakati huohuo
mafuta hayo yakiongezewa Shilingi 50 kwa kila lita.
Hili ni tatizo
kwa sababu wafanyabiashara wanaotumia mafuta hayo kwa kusafirishia mazao
au abiria kwenye magari yao au kwenye mitambo yao ni wazi kwamba
wataongeza bei tena maradufu hasa tukitilia maanani kwamba huwa hakuna
mtu anayewafuatilia.
Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), umeongezewa
kiasi cha Shilingi 186.9 bilioni ambazo awali hazikuwa zimetengwa
baada ya serikali kukubaliana na mapendekezo ya Bunge kupitia Kamati ya
Bajeti, inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Waziri
Mgimwa pia alitangaza kuanzisha kodi na ushuru katika huduma mbalimbali
zinazotolewa kupitia simu za mkononi, ikiwamo kodi ya zuio ya asilimia
10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha na imepandisha
viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari. Magari yenye ujazo wa
injini yenye ukubwa wa kati ya cc 501 na 1500 yatatozwa Shilingi 150,000
kutoka Shilingi 100,000, tukumbuke nayo hutumika sana na wananchi wengi
wa kawaida.
Ongezeko la vitu hivyo nilivyoviona mimi ni pigo kubwa kwa wananchi wa kawaida na hakuna nafuu yoyote, hivyo basi wabunge kazi ni kwenu!
Ongezeko la vitu hivyo nilivyoviona mimi ni pigo kubwa kwa wananchi wa kawaida na hakuna nafuu yoyote, hivyo basi wabunge kazi ni kwenu!
No comments:
Post a Comment