MWENYEKITI wa
Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi
iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013,
Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa
likiendelea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi
wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa
akiwania kuvaa taji la mkoa huo.
Mrembo aliyetimuliwa, Saphina Chumba akiwa jukwaani.
Hashimu Lundenga.
Lundenga alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kamati yake inataka kuendeleza nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili
na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi
ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima
ya Miss Tanzania.
Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na
kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu
wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.
Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.
Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.
Credit : GLP
No comments:
Post a Comment