Wanafunzi wanne
wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani
wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni
hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa
mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na
kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na
pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo,
wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na
majambazi kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.

Habari na FULLSHANGWE Blog.com
No comments:
Post a Comment