JESHI la Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni limeshindwa kumkamata
mkazi mmoja wa eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam, anayedaiwa kumbaka
mtoto mwenye umri wa miaka 12, (jina lake linahifadhiwa). Polisi wa
Kituo cha Magomeni jijini Dar es Salaam, ambako tukio hilo la ubakaji
liliripotiwa, wameshindwa kueleza sababu za kutomkamata mtuhumiwa licha
ya kujua mahali anapoishi.
Kwa mujibu wa mtu aliyebaini tukio hilo, alieleza kuwa lilitokea eneo la Magomeni Makuti, Aprili 21, mwaka huu ambapo mtoto huyo alibakwa na mume wa shangazi yake.
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wazazi wake wanaishi eneo la Kigamboni, lakini alichukuliwa na shangazi yake kwa ajili ya kuishi naye.
Mama mmoja anayeishi jirani na nyumbani kwa mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Halima, alilieleza gazeti hili kuwa alikutana na mtoto huyo usiku wa Aprili 21 kwenye daladala, akiwa njiani kwenda Kigamboni kwa mama yake mzazi.
Alisema alishangazwa na safari hiyo ya usiku, kutokana na umri mdogo wa mtoto huyo na jinsia yake na alipomdadisi alisimulia unyama aliofanyiwa na mume wa shangazi yake.
“Nilishangaa mtoto wa umri ule kusafiri kutoka Magomeni hadi Kigamboni usiku ule, nikamuuliza kama ametumwa akakataa lakini nilipombana akanieleza tukio zima. Nilipotaka kumrudisha nyumbani kwao alikataa akisema anaogopa kurudi huko, kutokana na uovu aliotendewa na mjomba wake.
“Kwa
kuwa mtoto yule si wangu nikaona si vema kulala naye nyumbani kwangu,
nilichokifanya ni kwenda kuripoti polisi ambao walikwenda kumchukua
mtuhumiwa, lakini hawakumfungulia kesi,” alisema.Kwa mujibu wa mtu aliyebaini tukio hilo, alieleza kuwa lilitokea eneo la Magomeni Makuti, Aprili 21, mwaka huu ambapo mtoto huyo alibakwa na mume wa shangazi yake.
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wazazi wake wanaishi eneo la Kigamboni, lakini alichukuliwa na shangazi yake kwa ajili ya kuishi naye.
Mama mmoja anayeishi jirani na nyumbani kwa mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Halima, alilieleza gazeti hili kuwa alikutana na mtoto huyo usiku wa Aprili 21 kwenye daladala, akiwa njiani kwenda Kigamboni kwa mama yake mzazi.
Alisema alishangazwa na safari hiyo ya usiku, kutokana na umri mdogo wa mtoto huyo na jinsia yake na alipomdadisi alisimulia unyama aliofanyiwa na mume wa shangazi yake.
“Nilishangaa mtoto wa umri ule kusafiri kutoka Magomeni hadi Kigamboni usiku ule, nikamuuliza kama ametumwa akakataa lakini nilipombana akanieleza tukio zima. Nilipotaka kumrudisha nyumbani kwao alikataa akisema anaogopa kurudi huko, kutokana na uovu aliotendewa na mjomba wake.
Mama huyu alieleza zaidi kuwa amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa baadhi ya askari wa kituo cha magomeni, wanaomuonya aache kujishughulisha na kesi hiyo kwa sababu inaweza kumsababishia matatizo.
“Pamoja na madai ya ubakaji kuthibitishwa na daktari wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Liwa, mtuhumiwa yuko huru na tukifuatilia tunazungushwa, sijui polisi kwa nini hawana utu kiasi hiki hata kwa watoto wadogo,” alisema.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Magomeni, Mwanne Salum, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema kwa mujibu wa sheria za jeshi hilo, yeye siyo msemaji hivyo atafutwe msemaji.
Na katika hali ya kushangaza, Afande Salum naye alimtaka mwandishi wa habari hizi kuacha kufuatilia suala hilo, huku akiahidi kuwa atalifuatia ili sheria ichukue mkondo wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alipoulizwa alisema hana taarifa za tukio hilo. “Ndio kwanza nasikia kutoka kwako, ila ningeomba huyo anayelalamika kwenye tuhuma hizo, aje ofisini kwangu nizungumze naye kwa ajili ya kujua kinachoendelea,” alisema Kenyela.
No comments:
Post a Comment