Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo.
Baada
ya mkutano na waandishi wa habari warembo walipata nafasi ya kutembelea
ofisi za wadhamini wao ambao ni Oriflame Natural Beauty Products
zilizopo jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam, na hapo waliweza kupata
semina ya kuelezewa jinsi vipodozi vyao vinavyofanya kazi kama pichani
unavyoona mwezeshaji akitoa somo kwa warembo.
Kila mrembo akijaribu kuweka kumbu kumbu kwa yale waliyokuwa wakifundishwa.
Mratibu
wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu
imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.
Ambapo mshindi wa kwanza
atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika
kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye
hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu aliyonayo. Pia
atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 300,000 pamoja na fedha
taslimu tshs. 500,000.Mshindi wa pili; atapata udhamini wa masomo
(Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 300,000 na shopping vocha
kutoka Oriflame ya tshs. 200,000.Mshindi wa tatu; atapata udhamini wa
masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping
vocha kutoka Oriflame ya tshs. 100,000.
Mshindi wa 4 na tano;
watapata uthamini wa masomo ya kompyuta ya miezi sita. Mshindi wa nne
atapata pia pesa taslimu laki mbili na nusu na wa 5 laki moja na
nusu.Washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha shilingi laki
mbili kwa kila mmoja. Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa
hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika
onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na
meza ya watu ukitazama zawadi. Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa
yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame
Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media
Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim
Blog, Sufian Mafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment