EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, June 19, 2013

Rombo: Wanafunzi Kidato cha Sita wabebeshwa mzigo wa Ualimu wa Sayansi.

KITENDO cha upungufu wa walimu wa sayansi nchini hasa katika shule za sekondari zinazomilikiwa na serikali kimezidi kuibua changamoto maeneo mbalimbali nchi.

Shule ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa ni sekondari za kata ambazo wingi wake umechochea zaidi changamoto hiyo.

Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto hiyo ya uhaba wa walimu wa sayansi kama ilivyo kwa mikoa tofauti ya Tanzania. Hata hivyo walimu wakuu wa shule zenye changamoto wamebuni mbinu mbadala kukabiliana na hali hiyo.

Zoezi la uhamasishaji ujenzi wa shule za sekondari za kata limekuwa na mafanikio kiasi kikubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, kwani hadi sasa wilaya hiyo imefikisha jumla ya sekondari 41 zilizo chini ya serikali ikiwa ni jitihada za wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao.
Mwandishi wa makala haya amefanikiwa kutembelea shule sita tofauti za sekondari za kata wilayani Rombo na kufanya mazungumzo na walimu wakuu, walimu na wananfuzi ambao wanatoa picha halisi ya uhaba wa walimu wa sayansi. Miongoni mwa shule zilizotembelewa ni pamoja na Sekondari za Nduweni, Tanya, Urauri, Holili na Ngaleku.Victus Kiwango ni Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Tanya iliyopo wilayani Rombo. Mwalimu huyu anasema uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni moja ya tatizo zinaloikabili shule hiyo. Kiwango anasema shule yake haina kabisa walimu wa masomo ya Kemia, Fizikia na Baiolojia hivyo hulazimika kutumia walimu wa kukodi kwa vipindi tofauti.

Anasema shule hiyo hutegemea wanafunzi kadhaa waliomaliza kidato cha sita ambao huwakodi na
PictureMwalimu Mkuu Msaidizi wa Nduweni Sekondari, Venance Mramba
kufundisha masomo hayo pale wanapopatikana ili wanafunzi waweze kupata chochote na hatimaye baadaye kufanya mitihani ya sayansi. "...Hapa shuleni kwetu (Tanya Sekondari) masomo ya sanyansi ndio tatizo, mfano hatuna kabisa walimu wa masomo ya Kemia, Fizikia pamoja na Baiolojia hivyo huwa tunakodisha na shule kuwalipa," anasema Kiwango.

Hata hivyo kero na kilio cha uhaba wa walimu kinasikika tena katika sekondari ya duweni wilayani humo.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa sekondari hiyo, Venance Mramba anasema tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi linaiathiri shule hiyo kitaaluma. Anasema shule miaka yote shule hiyo imekua ikianzia ufaulu wa daraja la pili.

Anatolea mfano katika matokeo ya mwisho ya kidato cha nne (juzi), ilifanikiwa kufaulisha mwanafunzi mmoja kwa daraja la pili na wanne kwa daraja la tatu. Anaongeza kuwa katika matokeo hayo wanafunzi 25 walipata daraja la nne na wanafunzi 70 wakiambulia sifuri, kati ya idadi ya wanafunzi 102 waliofanya mtihani huo wa mwisho wa taifa.

"Tatizo kubwa la kufaulu ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ikiwemo hesabu na mengineyo, uhaba wa vifaa vya ufundishaji na kujifunzia pamoja na upungufu wa vitatu vya masomo yote," anasema mwalimu Mramba katika mahojiano na mwandishi wa makala haya.

Anaongeza ili kukabiliana na upungufu wa walimu wa sayansi shule hiyo huajiri kwa muda wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na kuwasaidia kuwafundisha wanafunzi masomo hayo. Hata hivyo anasema bado kuna changamoto kubwa katika kuwatumia walimu hao wahitimu wa kidato cha sita, kwani hawana mbinu za kufundishia jambo ambalo bado ni kikwazo katika shule hiyo.

Benson Samizi ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Holili iliyopo katika Wilaya ya Rombo. Mwalimu huyu anasema japokuwa hali ya kitaaluma shuleni hapo si mbaya sana lakini shule inakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi kama ilivyo katika shule nyingine wilayani hapo.

Picture
Baadhi ya wanafunzi Sekondari ya Nduweni wakiwa darasani
Mwalimu Samizi anasema shule hiyo haina kabisa walimu wa masomo ya Fizikia na Hesabu na hulazimika kukodi walimu wa muda ili kuwaandaa wanafunzi. Shule hii haina maabara japokuwa ina vitabu vya kutosha vya masomo ya sayansi. Akizungumzia ufaulu wa kidato cha nne kwa mwaka 2011, anasema shule ilipata mwanafunzi mmoja aliyekuwa na daraja la kwanza na wengine wawili waliopata daraja la pili, huku wanafunzi watatu wakipata daraja la tatu.

Samizi anaendelea kubainisha kuwa katika matokeo hayo jumla ya wanafunzi 55 walipata daraja la nne na 18 kuambulia patupu (sifuri) kati ya watahiniwa 80 waliofanya mtihani wa mwisho wa taifa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2011.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Urauli, iliyopo Tarakea wilayani Rombo, Sim Silayo anasema mbali na biashara zinazofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo hilo kuathiri taaluma kimaudhurio, upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi ni kero nyingine shuleni hapo.

Mwalimu Silayo anaeleza kuwa shule hiyo haina kabisa walimu wa masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia; hivyo uongozi wa shule kulazimika kukodi walimu wa muda wa masomo ya sayansi wakiwemo baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita wanaosubiri kuendelea na masomo yao ya juu. Aidha anaongeza kuwa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007, yenye jumla ya wanafunzi 464 haina maabara wala vitabu vya kutosha licha ya kukabiliwa na changamoto zingine mbalimbali.

Yehova Mashalo ni mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Tanya anasema wapo wanafunzi wengi ambao hukata tamaa kuchukua masomo ya sayansi tangu wakiwa madarasa ya chini kutokana na kukosekana kwa walimu wa masomo hayo. Kwa upande wake Joice Kimaro mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Tanya anaongeza kuwa kutojitosheleza kwa walimu wa sayansi shule za sekondari hasa za kata inakatisha tamaa wanafunzi kupenda masomo hayo.
Picture
Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Urauri, Wilaya ya Rombo
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya anasema halmashauri yake inajitahidi kuongeza idadi ya walimu kila mwaka ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu. Anasema kwa uwiano wa kawaida Wilaya ya Rombo haina upungufu mkubwa wa walimu, lakini una upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi.

Anasema kwa sasa wilaya ina jumla ya walimu 800, huku kwa mwaka huu pekee ikiwa imeajiri walimu 134 wakiwemo wa masomo ya sayansi. "...Kwa suala la upungufu wa walimu Wilaya ya Rombo ni tofauti na maeneo mengine, hapa kuna upungufu wa walimu wa masomo; kama Hesabu, Fizikia, Kemia na Baiolojia nitatizo," anasema Mkurugenzi Mboya.

Hata hivyo anakiri kutokana na suala la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi zipo shule ambazo zimelazimika kutumia walimu wa kukodi na kutumia wanafunzi waliomaliza kidato cha sita ili shule iweze kwenda mbele. Anasema kuwa lengo kubwa la halmashauri hiyo ni kuhakikisha inatatua changamoto hiyo kila inapotokea nafasi.  

Kwa upande wake Katibu wa CWT Wilaya ya Rombo, Erasmo Mwingira anasema vijana wa kidato cha sita ambao hutumiwa na baadhi ya shule kuokoa jahazi la masomo ya sayansi wamekuwa hawafundishi zaidi ya kuwakaririsha wanafunzi kujibu mitihani jambo ambalo anatahadharisha huenda likawa na madhara makubwa kwa elimu yetu Tanzania.

"Kujua kusoma na kuandika si kigezo cha kumfundisha mtu...vijana hawa wa kidato cha sita hawana mbinu za ufundishaji, wanachokifanya ni kuwakaririsha wanafunzi," anasema Mwingira. Pamoja na hayo mdau huyu wa elimu anaishauri serikali kutojitoa katika jukumu la kuendesha shule za kata kwa kuwaachia wazazi kwani shule hizo ziko katika hali mbaya na zinahitaji kuongezewa fedha za uendeshaji.

*IMEANDALIWA na www.thehabari.com
Picture
Sehemu ya maktaba ya Sekondari ya Tanya, ikionesha utitiri wa vitabu vya sayansi japokuwa haina walimu wa somo hilo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate