Dodoma.
erikali imetoa kauli yake ya awali jana, kuhusu mlipuko wa bomu uliotokea katika Kata ya Soweto, mkoani Arusha wakati wa mkutano wa Chadema wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani mkoani humo.
erikali imetoa kauli yake ya awali jana, kuhusu mlipuko wa bomu uliotokea katika Kata ya Soweto, mkoani Arusha wakati wa mkutano wa Chadema wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani mkoani humo.
Shambulio hilo lilipoteza maisha ya watu wawili na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Tamko la Serikali kuhusu kadhia hiyo, lilitolewa jana bungeni na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi baada ya kipindi cha maswali na majibu.
“Sote tunajiuliza kwa nini wananchi waliwashambulia na kuwazuia askari wasitimize wajibu wao, badala ya kuwasaidia ili wamkamate mhalifu. Je, ilitokea kwa bahati mbaya au ilipangwa?” Waziri William Lukuvi
Katika tamko hilo, Serikali imevinyooshea kidole baadhi ya vyama vya siasa, taasisi za kijamii na watu binafsi (bila kutaja majina) kuwa vinahusika.
Lukuvi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huo ulikuwa wa bomu la kurushwa kwa mkono na kwamba aina ya urushaji wa bomu hilo hautofautiani na mbinu iliyotumika katika shambulio la Mei 5 mwaka huu katika Kanisa la Olasiti jijini Arusha.
Serikali pia imetangaza zawadi ya Sh100 milioni kwa watakaowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa na mtandao wao.
Zawadi hiyo inakuja huku Serikali ikiunda timu ya wataalamu wa kuchunguza tukio hilo.
Timu hiyo itaongozwa na Kamishna Paul Chagonja wa polisi ikishirikisha pia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
“Katika siku za karibuni, zimekuwepo jitihada za
makusudi za baadhi ya vyama vya siasa, makundi ya kijamii na watu
binafsi kupandikiza chuki kwa raia dhidi ya vijana wetu wa Jeshi la
Polisi, kuwafanya raia wawachukie askari, kuwafanya raia wasiwaamini
askari, kuwafanya raia wasiwape ushirikiano askari na hatimaye kuwa na
taifa ambalo halitawaliki,” alisema Lukuvi.
Alisema mlipuko huo ulikuwa wa bomu la kurushwa kwa mkono na kwamba lilirushwa kutoka upande wa Mashariki kuelekea Magharibi kulikokuwa na gari aina ya Fuso lililokuwa linatumika kuhutubia.
Kuhusu kutoroka kwa mtuhumiwa aliyerusha bomu
hilo, Lukuvi alisema ni matokeo ya uchochezi unaofanywa kwa makusudi na
baadhi ya wanasiasa dhidi ya Serikali na polisi.
“Sote tunajiuliza kwa nini wananchi waliwashambulia na kuwazuia askari wasitimize wajibu wao, badala ya kuwasaidia ili wamkamate mhalifu. Je, ilitokea kwa bahati mbaya au ilipangwa?”alihoji waziri huyo.
“Sote tunajiuliza kwa nini wananchi waliwashambulia na kuwazuia askari wasitimize wajibu wao, badala ya kuwasaidia ili wamkamate mhalifu. Je, ilitokea kwa bahati mbaya au ilipangwa?”alihoji waziri huyo.
Alisema shambulio hilo la Soweto limehama kutoka kanisani (Olasiti) kwenda kwenye mikutano ya kisiasa ikiwa na nia ya kuwafanya Watanzania wachukiane, wapigane na taifa liparaganyike.
Alisistiza kuwa baadhi ya wanasiasa kwa bahati mbaya au kwa
kujua na kushiriki mpango huo wamekuwa wakitoa kauli mfululizo za
kuendeleza chuki za kijamii wakidhani wanajiimarisha kumbe wanapanda
mbegu ya uharibifu kwa taifa.
“Serikali imepania kuwasaka na kuwatia mbaroni wahusika wa shambulio hilo la watu waovu. Kupitia Bunge hili nataka niwaambie wahalifu hao kuwa njama zao za kutugawa kwa misingi ya dini, makabila rangi, rasilimali na itikadi za vyama kuwa zitashindwa.
“Tutapambana nao usiku na mchana, kwa silaha zote
tulizonazo mpaka tutakapowashinda na kuwafikisha mbele ya mikono ya
sheria,” alisema.
Wabunge waomba mwongozo
Baada ya Lukuvi kuwasilisha kauli hiyo ya
Serikali, wabunge wanne wa vyama vya upinzani, Kombo Khamis Kombo (CUF),
David Kafulila, Felix Mkosamali na
Moses Machali wa NCCR-Mageuzi waliomba Mwongozo wa
Spika. Katika mwongozo wake, akitumia kanuni ya 47 Machali aliomba
Bunge liruhusiwe kujadili suala hilo akieleza kuwa kwa mujibu wa
mitandao ya kijamii inaonekana kuwapo kwa malumbano kati ya vyama vya
CCM na Chadema vikitupiana mpira kuhusu tukio hilo.
Alikwenda mbali zaidi na kutaka
kufanyika kwa uchunguzi na chama kitakachobainika kuhusika Msajili wa Vyama vya Siasa akifute.
Kwa upande wake, Kafulila alisema kauli ya Lukuvi inaashiria kwamba anajua sababu za tukio hilo.
Kombo aliitaka Serikali itoe maelezo kuhusu
matukio kama hilo yaliyotokea Zanzibar, akisema ukimya wa Serikali
unawafanya wananchi kutoielewa.
Spika Makinda
Hata hivyo baada ya wabunge hao kuomba mwongozo,
Spika wa Bunge Anne Makinda alisema kuwa kutokana na uzito wa tukio hilo
ameitisha kikao cha Kamati ya Uongozi kujadili suala hilo.
No comments:
Post a Comment