Wachezaji
wa Taifa Stars wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo katika mchezo
wa kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Ivory Coast. Stars
ilifungwa 4-2.
............................................................................................................
Kocha
wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4
mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini
Afrika Kusini.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo
(Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C
Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kim
amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi
sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe
Englebert.
Wachezaji
hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally
Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir,
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba,
Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri
Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Mechi
hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es
Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano
itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole
nje kidogo ya Jiji la Kampala.
MECHI DHIDI YA IVORY COAST YAINGIZA MIL 500/-
Mechi
ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16
mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji
tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.
83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 20,886,282.09.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25
ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment