Jumla ya vitanda 15 vyenye thamani ya
shilingi milioni 52.5 zimepatikana katika harambee iliyoandaliwa na
warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 kwa ajili ya kununua vitanda kwa
ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za
Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina iliyofanyika katika ukumbi wa
Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mshiriki wa shindano hilo, Sarah Paul alisema kuwa wanamshukuru Mungu
kwa kuweza kuwawezesha kufanya harambee hiyo ambayo ilitokana na wao
baada ya kutembelea hospitali ya Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina
wakajionea uhaba wa vitanda vya akina mama wakati wa kujifungua.
“Tulisononeshwa
sana na hali tuliyoikuta hospitalini hapo ambapo baada ya kuongea na
mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni dokta Gunini Kamba alitueleza kuwa
jumla ya akina mama wapatao 50 mpaka 80 hujifungua kwa siku moja hivyo
wanauhaba wa vitanda, tukaona tukae na viongozi wetu watusaidie kuandaa
harambee na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata vitanda 15 japo nia
yetu ilikuwa ni kupata vitanda 20,” alisema mrembo huyo.
Mashindano
ya Redd’s Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa
hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika
onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na
meza ya watu ukitazama zawadi.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakitambulishwa kwa Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Mgeni huyo pia alipata fulsa ya kuzinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 walipata fulsa ya kucheza mara baada ya harambee na ufunguzi rasmi ya kambi yao.
Furaha zilitanda.
Kila mmoja akionyesha ufundi wake.
Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment