Serikali imetangaza bajeti yake ya mwaka 2013/14 na kupandisha ushuru wa mafuta ya petroli na dizeli kwa Sh200.
Katika bajeti ya mwaka 2012/2013, Serikali ilieleza hatua ilizochukua kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi kwa lengo la kupunguza makali ya maisha kunakotokana na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma.
Ilieleza hatua zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na kurekebisha namna ya kukokotoa gharama za mafuta na kutangaza bei elekezi kila mwezi na kuanzisha utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja.
Akisoma bajeti hiyo jana mjini Dodoma, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, alisema mafuta ya dizeli ushuru wake umepanda kutoka Sh215 kwa lita hadi Sh217 ikiwa ni ongezeko la Sh 2 tu.
“Mafuta ya petroli kutoka kiwango cha sasa Sh339 kwa lita hadi Sh400 kwa lita,” alisema.
Alifafanua kwamba mafuta ya taa ushuru wake umebaki kuwa Sh400.30.
Hata hivyo baadhi ya wananchi, wameelezea hisia zao kuhusu bajeti hiyo wengi wakidai kuwa inawazidishia ugumu wa maisha.
SDL ni kodi ambayo hulipwa na waajiri kulingana na idadi ya waajiriwa wake,fedha ambazo hupelekwa kwenye taasisi za elimu ya ufundi na ile ya juu.
Kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2011, katika asilimia sita ya fedha zilizokuwa zinalipwa na taasisi asilimia nne zilikuwa zinapelekwa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu na asilimia mbili, na Veta. Katika hotuba yake ,Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa,alisema sambamba na kupunguza kiwango hicho taasisi za Serikali zisizotegemea bajeti ya Serikali kwa kiwango kikubwa katika kujiendeleza kitalipa tozo hiyo.
Hoja ya kupunguzwa kwa tozo hiyo na kupanua wigo wake iliyolewa na kambi ya upinzani wakati wa bajeti ya mwaka 2012/13.
Hotuba hiyo iliyosomwa na Waziri Kivuli wa Fedha Zitto Kabwe, alipendekeza tozo hiyo kupunguzwa kutoka asilimia sita mpaka asilimia nne.
Lengo ni kupunguza mzigo kwa waajiri na kuondoa ubaguzi kwani wanaofaidika na tozo hii pia huajiriwa na Serikali na Mashirika ya Umma.”
Wigo wa kodi wapanuka
Serikali imepunguza Tozo ya Kuendesha Mafunzo ya Ufundi Stadi (skills development levy ‘SLD’) kutoka asilimia sita mpaka tano na kutanua wigo wa ulipaji wa kodi ambapo sasa mashirika ya umma pia yatailipia.SDL ni kodi ambayo hulipwa na waajiri kulingana na idadi ya waajiriwa wake,fedha ambazo hupelekwa kwenye taasisi za elimu ya ufundi na ile ya juu.
Kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2011, katika asilimia sita ya fedha zilizokuwa zinalipwa na taasisi asilimia nne zilikuwa zinapelekwa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu na asilimia mbili, na Veta. Katika hotuba yake ,Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa,alisema sambamba na kupunguza kiwango hicho taasisi za Serikali zisizotegemea bajeti ya Serikali kwa kiwango kikubwa katika kujiendeleza kitalipa tozo hiyo.
Hoja ya kupunguzwa kwa tozo hiyo na kupanua wigo wake iliyolewa na kambi ya upinzani wakati wa bajeti ya mwaka 2012/13.
Hotuba hiyo iliyosomwa na Waziri Kivuli wa Fedha Zitto Kabwe, alipendekeza tozo hiyo kupunguzwa kutoka asilimia sita mpaka asilimia nne.
Lengo ni kupunguza mzigo kwa waajiri na kuondoa ubaguzi kwani wanaofaidika na tozo hii pia huajiriwa na Serikali na Mashirika ya Umma.”
No comments:
Post a Comment