HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde
imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Usafiri Dar es
Salaam (UDA), Idd Simba, Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa
Kata Sinza(CCM), Salum Mwaking’inda, Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor
Milanzi na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer
Feleshi kuwasilisha hati ya
kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya
kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka
2002.
Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa
na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka jana wakikabiliwa
na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na
hujumu uchumi.
No comments:
Post a Comment