Baada ya wadau mbalimbali kuanza kuhoji kuhusu uhalisia wa
safari za mwigizaji Jennifer Kyaka (Odama) kwenda ulaya ambaye picha
zake kadhaa zilizotolewa mtandaoni wiki chache zilizopita zikimtuhumu
kuwa huwa haendi nje ya nchi bali anakuwepo nchini kwa lengo la
kutafuta “kiki” na kutengezeza picha hizo kwa program maalumu ya
kompyuta, hatimaye jana kupitia mtandao mmoja wa kijamii aliweka
picha zake mpya zinazomuonesha nchini Qatar katika maduka mbalimbali na
kwenye uwanja wa ndege wa nchi hiyo.
Picha hizi zimekuja kama ushahidi na majibu ya mwaswali
yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wengi kuhusu mwanadada huyu. Tazama picha
hizi hapo
CREDIT: BONGO MOVIE
No comments:
Post a Comment