MWIGIZAJI mahiri Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Jumatano iliyopita
alizua hekaheka mtaani baada ya kutinga kwenye duka moja na watu
kumtumbulia macho kwa kumshangaa.
Tukio
hilo lilitokea kwenye duka hilo lililopo Sinza Afrika Sana ambapo staa
huyo mwenye kesi ya madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa staa wa
filamu za Bongo, marehemu Steven Kanumba, alitinga dukani hapo akihitaji
huduma ya fedha kwa njia ya mtandao wa simu.
Baadhi ya watu
waliokuwa wanapita jirani, walimkodolea macho Lulu huku kila mtu akisema
lake. Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina, alisikika akisema:
“Ametulia siku hizi, tangu ametoka Segerea amekuwa mtulivu sana.”
Baada ya kuhudumiwa, Lulu alitoka lakini baadaye akagundua kuwa amesahau funguo ya gari, hali iliyomlazimu kurudi dukani.
Baada ya kuhudumiwa, Lulu alitoka lakini baadaye akagundua kuwa amesahau funguo ya gari, hali iliyomlazimu kurudi dukani.
Aliporudi
dukani, aliiona funguo hiyo, akatoka na kwenda kwenye gari alilokuja
nalo. Ndani ya gari hilo aina ya Toyota Mark II, alikuwa na mdogo wake
ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Credit: GLP
No comments:
Post a Comment