Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, amesema
kuwa, kuna hatari ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwa Tanzania Bara
kutofanyika ikiwa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa
na Tume ya Katiba yatapita kama yalivyo.
Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Makinda ambaye pia ni Mbunge wa
Njombe Kusini (CCM) amesema kwamba, ikiwa mapendekezo hayo yatatipishwa
na wananchi kama yalivyo, Tanzania Bara haitaweza kuingia katika
uchaguzi kwa vile haitakuwa na katiba.
Wakati Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania akizungumza hayo, tayari Tume ya Mabadiliko ya
Katiba imeshatangaza kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya mabaraza
kuanzia Julai 12 hadi Agosti 2, mwaka huu.
Spika Makinda amewataka
Watanzania kuisoma rasimu ya Katiba hiyo hiyo vizuri na kuonyesha
wasiwasi wake juu ya taifa la Tanzania kuwa na serikali tatu. Makinda
amesema kwa mshangao juu ya maoni ya kuwa na serikali tatu na kusema,
nchi hii itakuwa na marais watatu, maspika watatu, mabunge matatu,
majeshi matatu na benki kuu tatu.
Chanzo cha habari ni Idhaa ya kiswahili Tehran
No comments:
Post a Comment