MIMBA ya mrembo Lisa Jensen ambayo sasa haina kificho kutokana na
ukubwa wake, inaonekana kumtesa ile mbaya na kumfanya abadili mfumo wa
maisha yake.
Rafiki
wa karibu wa Lisa aliyeomba hifadhi ya jina lake hivi karibuni
aliliambia gazeti hili kuwa, ujauzito alionao mlimbwende huyo unampa
wakati mgumu hasa ikichukuliwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kuwa na hali
hiyo.
“Kiukweli
mimba inamtesa, si unajua na ule ulainilaini wake halafu ndiyo kwanza
anashika ujauzito kwa hiyo hata ule usistaduu wa kivile sasa hana,
anafikiria siku atakapojifungua na kuitwa mama,” alisema mtoa habari
huyo.
No comments:
Post a Comment