EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, July 14, 2013

VITUO VYA WATOTO YATIMA KUNUFAIKA MSIMU WA RAMADHAN.

Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, akikabidhi sabuni, mafuta na vitabu kwa watoto yatima kati ya 700 wa madrasa Kisarawe, wakati wa futari ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, walioambatana na Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi milion 50 kwa ajili ya kipindi hiki cha Ramadhan.
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, akikabidhi mbuzi kwa mmoja wa watoto yatima kati ya 700 wa madrasa Kisarawe, wakati wa futari ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya kipindi hiki cha Ramadhan.
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, akimsikiliza Mwenyekiti wa bodi wa Vodacom Foundation Hassan Saleh, akimfafanulia jambo wakati wa futari na baadhi ya watoto yatima kati ya 700 wa madrasa Kisarawe, iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia  kampeni yake ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi milion 50 kwa ajili ya kipindi hiki cha Ramadhan.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwapa vyakula baadhi ya watoto wa madrasa wanaoishi katika mazingira magumu Kisarawe Pwani  wakati wa futari iliyaoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom iliyotenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani  na kuudhuriwa na Mgeni rasmi Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi hayupo pichani.
KISARAWE-PWANI Katika kipindi hiki cha msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani vituo mbalimbali vya watoto yatima hupata misaada kutoka taasisi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwa pamoja na kuwafarij wagonjwa na watoto waishio katika mazingira magumu.

Vituo vingi vimekuwa vikikabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu na maradhi kwa watoto wanaokaa au kulelewa katika vituo hivyo, na katika msimu huu wa ramadhani ambao mara nyingi uhitaji wa chakula kinachokidhi haja ya watoto wanaoishi katika vituo hivyo huwa ni mkubwa kutokana na aina ya vyakula vinavyo hitajika kufuturu.

Kutokana na kukabiliana na changamoto zinazovikabili vituo hivyo kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wa huduma za jamii wamezindua mpango wa Pamoja na Vodacom ambao utawezesha vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima na wengine waishio katika mazingiza magumu wakipata msaada wa chakula na maradhi katika kipindi hiki cha msimu wa Ramadhan.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Kisarawe, Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa kitengo cha huduma za jamii “Vodacom Foundation”, Hassan Saleh alisema kuwa mpango huu ambao umedumu kwa miaka sita hadi sasa utashuhudia vituo kadhaa nchini vikipata msaada wa chakula, nguo, madawa pamoja na vifaa vya kujifunzia.

 “Hiki ni kipindi muhimu kwa ndugu zetu waislam kwa kuwa karibu zaidi na Mungu, lakini pia kipindi hiki kinatoa fursa kwa watu mbalimbali kujumuika na wagonjwa pamoja na watu wengine waishio katika mazingira magumu na kuwa pamoja nao, kuwafariji na kuwasaidia mahitaji yao mbalimbali,” alisema Saleh, na kuongeza kuwa.

“Kwetu sisi kupitia mfuko wetu wa huduma za jamii tumejiwekea mpango huu wa kuhakikisha tunawaunga mkono wale wote wanaojumuika na makundi haya kuhakikisha tunawafariji na kuwapatia mahitaji yote muhimu katika kipindi hiki cha msimu wa Ramadhani.”

“Kwa kuanzia katika mpango huu, tutashuhudia zaidi ya watoto 700 kutoka katika vituo mbalimbali vya mkoa wa pwani wakipata misaada hii na baada ya hapo tutaenda katika mikoa mingine ya bara na visiwani,” alisema Saleh.

Rais wa Zamani wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa juhudi zake za kuwasaidia Watanzania kwa njia mbalimbali.

“Ni furaha yetu kuona jinsi ambavyo mnaendela kuwasaidia wananchi wa Tanzania. Tunawatakia kila la kheri katika majukumu yenu ya kila siku,” alisema rais huyo wa zamani.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate