Stori: Chande AbdallahMsanii
wa filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amesema anamtakia mafanikio
mema kinda la filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kujitangaza
kuwa amebadilika.

Akizungumza na paparazi wetu, Dk. Cheni alisema amefurahi kusikia
mikakati ya Lulu na kumsihi ajitahidi kuishi hivyo ili aweze kufikia
malengo yake kama alivyojipangia.

“Kwanza nampongeza na namuombea kwa Mungu atimize malengo yake. Ni
jambo zuri kama ameamua kujikita katika kazi zaidi ya kitu chochote,”
alisema Dk. Cheni.
No comments:
Post a Comment