MSHAHARA wa watumishi wa ndani, sasa umewekwa kisheria kuanzia Julai mosi, kupitia tangazo la Serikali la Kima cha Chini cha Mshahara wa Kisekta, lililotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililochapishwa jana katika vyombo vya habari, wafanyakazi wote wa ndani walioajiriwa, mbali na wanaofanya kazi za ndani kwa makubaliano mengine yasiyo ya ajira, kama muda mfupi na kuacha, wanapaswa kulipwa si chini ya kiwango kilichotajwa kisheria.
Watumishi hao wamepangwa kwa madaraja, ambapo daraja la kwanza litahusu watumishi wa ndani katika nyumba za waajiri wenye hadhi ya kibalozi na wa mashirika ya kimataifa.
Daraja hilo la kwanza litahusu pia watumishi wa ndani katika nyumba za wafanyabiashara mashuhuri, ambao kwa pamoja watalipwa kwa mwezi si chini ya Sh 150,000, ambayo ni sawa na Sh 34,618 kwa wiki, Sh 5,769.70 kwa siku na Sh 769.30 kwa saa.
Watumishi katika nyumba za maofisa wenye nafasi za juu, watakuwa daraja la pili na kulipwa si chini ya Sh 130,000 kwa mwezi, sawa na Sh 30,002.30 kwa wiki, Sh 5,000.40 kwa siku au Sh 666.70 kwa saa.
Katika daraja la tatu, kima cha chini kinahusu watumishi wa ndani ambao wanafanyakazi kwa watu wengine mbali na maofisa wenye hadhi ya kibalozi, wafanyabiashara mashuhuri na maofisa wa juu.
Watumishi hao ni wanaofanya kazi na kuondoka jioni, ambao mshahara wao wa kima cha chini kwa mwezi utakuwa si chini ya Sh 80,000, sawa na Sh 18,463 kwa wiki na Sh 3,077.15 kwa siku au Sh 410 kwa saa.
Daraja la mwisho ni kwa wafanyakazi wengine wa ndani, ambao mshahara wao wa kima cha chini, utakuwa si chini ya Sh 40,000.
Watumishi hao mapato yao hayajatafsiriwa kwa wiki, siku au saa lakini ndio wanaolipwa kima kidogo kuliko sekta zingine nchini. Sekta nono Sekta zilizoongoza kwa kuwa na kima cha chini cha mshahara, ambacho ni kikubwa kwa mwezi, ni sekta ya mawasiliano ya simu, huduma za kifedha, migodi iliyothibitika kuwa na madini, na kampuni za kimataifa za nishati ambazo kima cha chini ni Sh 400,000 kwa mwezi.
Sekta zinazofuata kwa kuwa na kima cha chini chenye mshahara mnono kwa mwezi ni sekta ya ujenzi kwa kampuni za ujenzi za daraja la kwanza, ambayo kima cha chini ni Sh 325,000.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyakazi katika usafiri wa anga, kampuni za upakiaji na upakuaji mizigo na kampuni zinazotafuta madini, kima cha chini kinapaswa kuwa Sh 300,000.
Watumishi katika kampuni za ujenzi daraja la pili mpaka la nne, watalipwa si chini ya Sh 280,000, wakifuatiwa na watumishi wa kampuni za ujenzi daraja la tano mpaka la saba na wa hoteli za kitalii ambao kwa mwezi kima cha chini kimetajwa kuwa Sh 250,000.
Kwa wafanyakazi wa kampuni za usafirishaji za majini na nchi kavu, wakiwemo madereva na makondakta wa daladala na kampuni za uvuvi, kima cha chini kitakuwa Sh 200,000.
Wafanyakazi katika kampuni za habari, posta na usafirishaji wa vifurushi na kampuni za kimataifa za ulinzi, kampuni ndogo za kuzalisha nishati na hoteli za kati, kima cha chini kitakuwa Sh 150,000, kikifuatiwa kwa karibu na kima cha chini kwa shule binafsi za sekondari mpaka chekechea, ambacho ni Sh 140,000.
Katika sekta ya afya, kima cha chini kitakuwa Sh 132,000, kikifuatiwa na hoteli, nyumba za kulala wageni na baa Sh 130,000, biashara na viwanda, sekta ya kilimo na zingine ambazo hazijatajwa itakuwa Sh 100,000.
Likizo “Kima cha chini kama kilivyoainishwa, kitatafsiriwa kama kiwango cha chini cha mapato atakayopewa mwajiriwa katika sekta husika. Mwajiri anaweza kumlipa mwajiriwa mapato ya juu zaidi, lakini hapaswi kulipa chini ya mapato yaliyowekwa na sheria.
“Mwajiriwa pia anastahili kupata likizo ya malipo kila mwaka na posho ya usafiri mara moja kila baada ya miaka miwili ya kufanya kazi kwa mwajiri mmoja,” ilifafanua sheria hiyo.
Sheria hiyo pia inamtaka mwajiri ambaye anamlipa mtumishi wake vizuri kuliko kima cha chini kilichotangazwa, aendelee kumlipa mapato hayo na mafao mengine anayostahili. Pamoja na tangazo hilo, tayari kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya kada ya watumishi kulipwa kiasi kidogo cha mishahara na hivyo kuwafanya washawishike kuiba na wengine kujiuza.
Kada ya watumishi wa baa na nyumba za kulala wageni na huduma zifananazo na hizo, wamekuwa waathirika wa malipo hayo ya chini na hata kupunjwa au kudhulumiwa na waajiri wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment