Baada ya kupata ajali ya gari jana alipokuwa akimrudisha rafiki
yake Gelly wa rhymes (Mwanamuziki wa bongofleva) nyumbani kupitia
ukurasa wake wa mtandao kijamii mwigizaji na mwanamuziki Hemedy Suleiman
amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa anaendelea vizuri licha ya
ajali iliyomkuta.
Akiandika Hemedy amesema
“NAMSHUKURU MUNGU NAENDELEA VIZURI LICHA YA AJALI MBAYA
ILIYONIKUTA..Ahsante kwa dua zenu..KIFUA TU NDIO KIMEUMIA SANA NA
MKONO...”
Tunafanya mawasiliano zaidi na Hemedi kwa taarifa zaidi za chanzo cha ajali hiyo na tutawajulisha zitakapo kuwa teyari.
(Picha: gari alilopata nalo ajali Hemedi)
No comments:
Post a Comment