BAADA ya kuwekewa vizingiti katika kazi yake ya usambazaji wa filamu,
Mkurugenzi wa Kampuni ya 5 Effect, William Mtitu amesema anamshukuru
Mungu kwani ameishinda vita hiyo.
“Najivunia kwamba
nimeshinda vita maana jamaa walikuwa wakinifanyia mchezo mchafu. Kila
nilipotangaza kutoa filamu na wao wakawa wanaingiza filamu mpya lakini
nashukuru Mungu kwamba sasa hivi nimeweza.
“Huwezi kuamini,
nilipoingiza sokoni Omega ndani ya masaa matano nililazimika kuongeza
nakala nyingine kwani inanunuliwa kama karanga,” alisema Mtitu
No comments:
Post a Comment