KIPA namba moja wa Taifa
Stars, Juma Kaseja dili lake la kwenda kuichezea FC Lupopo ya DR Congo
halieleweki na kusisitiza kuwa ameamua kujiunga na timu ya Ndanda FC
inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa ajili ya mazoezi ili kujiweka
fiti kipindi hiki ambacho hana timu.
Akizungumza na Championi
Ijumaa, Kaseja ambaye alimaliza mkataba wake na Simba msimu uliopita,
alisema kabla ya kusafiri na timu ya taifa, alikuwa akifanya mazoezi na
timu hiyo, ingawa anaendelea kufanya mazoezi kwa manufaa ya afya yake.
Aliongeza kuwa, suala la usajili wa Lupopo hapendi kulizungumzia kwa
sasa kwa kuwa yeye bado ni mchezaji huru, lakini baada ya Ndanda
kuondoka kwenda Mtwara juzi Jumatano, amejikita zaidi kuendesha shughuli
zake binafsi.
“Nimekuwa nikifanya mazoezi na Ndanda, lakini baada
ya kuondoka, ninaendelea na shuguli zangu binafsi, siyo lazima kuzijua,”
alisema Kaseja huku akiwa hayupo tayari kufafanua kwa undani juu ya
usajili wake wa kwenda Lupopo.
Ndanda ilikuwa jijini Dar es Salaam
ambapo ilicheza mechi za kirafiki dhidi ya Saigon ya Mwananyamala na
Ruvu Shooting ya Pwani, ambapo itaanza kucheza mechi za Daraja la Kwanza
keshokutwa Jumapili dhidi ya Friends Rangers kwenye Uwanja wa
Nang’wanda, Mtwara.
CREDIT GLP
No comments:
Post a Comment