Akihutubia katika mkutano wa hadhara leo uliofanyika mjini Lamadi Busega Kinana ametoa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Serikali za Mitaa TAMISEMI Hawa Ghasiapamoja na watendaji wengine wa Serikali katika sekta ya Elimu kuhakikisha wanashughulikia kero za walimu hasa katika malipo yao mbalimbali ili kumaliza tatizo la malimbikizo hayo, Kinana amesema kama watendaji hao wa serikali hawatamaliza tatizo hilo atawashughulikia kwa kuwashitaki kwa wabunge wa CCM ili wawawajibishe kwa kukiuka agizo la Rais Dr.Jakaya Kikwete ambaye aliagiza watendaji hao kumaliza matatizo ya walimu, Katika picha katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Besega Ndugu Paul Mzindakaya na aliyenyanyua mkono kushoto ni Mbunge wa jimbo la Busega Dr. Titus Kamani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika kata ya kabita wilayani Besega.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti kulia akizungumza jambo na Mkuu
wa wilaya ya Besega Paul Mzindakaya kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Lamadi Busega.
Kikundi cha ngoma cha lamadi Busega kikitumbuiza katika mkutano huo.
Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara wakifuatilia matukio ya mkutano huo.
Katibu
wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akuhutubia wananchi
katika mkutano huo wa hadhara mjini Lamadi wilayani Busega.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Lamadi Simiyu.(PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-LAMADI SIMIYU)
No comments:
Post a Comment