KOCHA David Moyes ameonyesha nini
alihitaji kucheza soka ya wazi, soka adimu Uwanja wa Old Trafford,
ambayo matunda yake ni kushinda mabao mengi, 4-2 dhidi ya Bayer
Leverkusen ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi Ligi
ya Mabingwa usiku huu.
Rooney akishangilia
Hadi
sasa, Moyes wakati wote amekuwa akijaribu kuwatumia pamoja Robin van
Persie na Wayne Rooney pale mbele. Sasa wako upande wake na wanamfanyia kazi nzuri.
Van
Persie amefunga moja ya mabao ya msimu, Rooney amefunga mawili na
lingine Antonio Valencia katika ushindi ho na sasa wanaelekea kwenye
mchezo dhidi ya mahasimu wao, Manchester City wakiwa wenye kujiamini.
Faraja
kwa Rooney leo ametimiza mabao 200 ya kuifungia United, hivyo kuingia
kwenye orodha ya magwiji wa klabu, Bobby Chartlon mabao 249, Dennis Law
237 na Jack Rowley 211.
Kitu hicho: Rooney akimtungua kipa wa Leverkusen, Bernd Leno
Anapongezwa: Rooney akishangilia na Chris Smalling na Michael Carrick baada ya kufunga bao la kwanza
Anamtesa kipa: Rooney akimzunguka kipa wa Leverkusen, Leno kipindi cha pili
... lakini Rooney alikosa bao la wazi baada ya kupiga shuti lake huku Van Persie akishuhudia
Nimefanyaje? Rooney akishika kichwa chake kusikitika baada ya kukosa bao la wazi
Hata kocha hakuamini: David Moyes hakuamini kama Rooney amekosa bao la wazi, hata Sir Alex Ferguson (chini) pia hakumini
Ngumu kuamini: David Moyes hakuamini, hata Sir Alex Ferguson pia
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Damir Skomina wa Slovenia, Rooney alifunga dakika ya 22 na Bayer wakasawazisha kupitia kwa Rolfes dakika ya 54, kabla ya Van Persie kufunga la pili dakika ya 59, Rooney tena la tatu dakika ya 70 na Valencia dakika ya 79 kabka ya wageni kupata bao la pili dakika ya 88 kupitia kwa Toprak.
Kikosi
cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra,
Valencia, Carrick, Fellaini/Cleverley dk81, Kagawa/Young dk71,
Rooney/Hernandez dk84 na Van Persie.
Bayer
Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Toprak, Boenisch, Can, Reinartz,
Rolfes, Sam/Kruse dk78, Kiessling/Derdiyok dk78 na Son/Benderdk 64.Uteuzi wa timu wa Moyes unamaanisha Ryan Giggs atasubiri sana kuongeza idadi ya mabao yake.
Mkongwe
huyo wa United, akiwa amebakiza miezi miwili kusherehekea kutimiza
miaka 40, amefungana kwa na gwiji wa zamani wa Real Madrid, Raul katika
kucheza mechi nyingi katika Ligi ya Mabingwa, wote 144).
Na kwa kuwa Giggs hakuwepo hata benchi, kuna uwezaekano ikamchukua muda sana.
Giggs
na Raul wanafuatiwa na Paolo Maldini (mechi 140), Xavi (mechi 136),
Clarence Seedorf (mechi 131), Paul Scholes (mechi 130) na Iker Casillas
(mechi 129).
SIKU YA ROONEY...LAKINI GIGGS MAJANGA
Uteuzi wa timu wa Moyes unamaanisha Ryan Giggs atasubiri sana kuongeza idadi ya mabao yake.
Mkongwe
huyo wa United, akiwa amebakiza miezi miwili kusherehekea kutimiza
miaka 40, amefungana kwa na gwiji wa zamani wa Real Madrid, Raul katika
kucheza mechi nyingi katika Ligi ya Mabingwa, wote 144).
Na
kwa kuwa Giggs hakuwepo hata benchi, kuna uwezaekano ikamchukua muda
sana. Giggs na Raul wanafuatiwa na Paolo Maldini (mechi 140), Xavi
(mechi 136), Clarence Seedorf (mechi 131), Paul Scholes (mechi 130) na
Iker Casillas (mechi 129).
Bonge la bao: Robin van Persie (kushoto) akifunga bao safi
Bao tamu: Robin van Persie (kulia) akifunga moja ya mabao bora ya msimu
Mholanzi kiwango: Van Persie akiwapa ishara mashabiki Uwanja wa Old Trafford baada ya kufunga bao zuri
La pili: Rooney akifunga bao lake la pili usiku huu na kufikisha mabao 200 United - hapa anamtenda tena Leno
Kijana wa kihistoria: Rooney akiruka hewani kushangilia baada ya kufunga bao la 200 United
Mtaalamu: Antonio Valencia akifumua shuti kuifungia United bao la nne
Imetulia mwaka: Van Persie akimpongeza Valencia baada ya kuhitimisha mvua ya mabao ya United
Kifaa kipya: Marouane Fellaini (kulia) amecheza mechi ya kwanza kamili United
Mabao ya wageni: Simon Rolfes (juu) na Omer Toprak (chini) waliifungia Leverkusen
No comments:
Post a Comment