EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, September 11, 2013

Profesa Maina auponda muundo wa Bunge la Katiba..Bunge haliwajibiki.

Dar es Salaam. 
Mwanasheria maarufu, Profesa Chris Peter Maina ameuponda muundo wa Bunge la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kushauri utizamwe upya kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni mwakani.

Profesa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, alisema kama hilo lisipofanyika inaweza kupatikana Katiba Mpya yenye mlengo wa chama kimoja cha siasa na kufafanua kuwa tatizo hilo limetokana na upungufu katika sheria ya mabadiliko ya Katiba ambayo imefanyiwa marekebisho kidogo na kupitishwa na wabunge mjini Dodoma wiki iliyopita.

“Vyama vya siasa vinaweza kujipanga na kuweka watu wao katika zile nafasi 166 za wawakilishi wa kawaida katika Bunge maalumu la Katiba, hapohapo kumbuka kuwa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanaingia katika Bunge hilo,” alisema.

Wakati Profesa Maina akieleza hayo, Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Palamagamba Kabudi alisema, kazi ya tume hiyo itaishia katika Mabaraza ya Katiba na kwamba katika hatua nyingine za Bunge la Katiba na kura ya maoni haitahusika.

Kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge la Katiba litakuwa na wabunge 604 na wawakilishi 81 ambapo uwakilishi mkubwa utatoka katika vyama vya siasa huku CCM wakiwa na wabunge 398 sawa na asilimia 66 na upinzani wabunge 206 sawa na asilimia 34.

Alhamisi iliyopita wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, muswada ambao haukuungwa mkono na wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kwa madai kuwa umejaa makosa mengi.

Kambi ya upinzani walitaka muswada huo usitishwe,huku wabunge wa CCM wakipinga,hali ambayo iliibua vurugu.

Wapinzani walikuwa wakipinga mambo kadhaa ikiwa ni kutokushirikishwa katika kutoa maoni kwa Wazanzibari na suala la Rais kupewa madaraka ya kuteua wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba.

Akizungumza jana katika kongamano la Katiba lililoandaliwa na Jukwaa la Katiba (Jukata), Profesa Maina alisema ikiwezekana wabunge wanatakiwa kuelimishwa juu ya ushiriki wao katika bunge hilo ili watambue kuwa wanachokwenda kukifanya siyo kwa ajili ya kuwaondoa wao bungeni, bali ni kwa ajili ya Tanzania ya zaidi ya miaka 50 ijayo.

“Ukikosekana moyo wa dhati wabunge wanaweza kuizuia Katiba, inawezekana kabisa vikaingiza watu wao.

Tatizo lilikuwa katika sheria ya mabadiliko ya Katiba, nadhani watu walikuwa na haraka ya kwenda katika mchakato huo. Katiba Mpya inapatikana katika Bunge la Katiba huo ndiyo wasiwasi wangu,” alisema.

Alisema kuwa Bunge hilo haliwajibiki kufuata Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba linaweza kuweka mambo yao wenyewe.

Profesa Kabudi alisema, kati ya hatua nne za kupata Katiba Mpya, hatua mbili ndiyo zinaihusu Tume ya Katiba moja kwa moja ambazo ni kukusanya maoni ya wananchi na makundi maalumu pamoja na Mabaraza ya Katiba, “Tume haitahusika katika Bunge la Katiba na kura ya maoni.”


Alisema katika utoaji wa maoni ya Katiba Watanzania walionyesha wazi kutotaka kuchezewa kwa miiko ya uongozi, uwajibikaji, maadili ya uongozi, uwazi, haki, usawa na amani, huku akisisita kuwa vitu hivyo ni vya msingi katika mustakabali wa nchi.

Alisema hata masuala yaliyotolewa maoni na wananchi lakini hayakuingizwa katika rasimu yanayohusu sera, sheria na utekelezaji yameorodheshwa na tume itawapatia viongozi ili wayasome.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alisema mpaka sasa rasimu ya pili ya Katiba bado haijaandaliwa wakati Bunge la Katiba limepangwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu.
“Tunataka kujua itachukua muda gani mpaka kupata rasimu hii ya pili. Hatujaridhishwa na marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba, hayana mashiko kwani uteuzi wa wajumbe 166 pamoja na uteuzi wa rais ni moja ya kasoro kubwa,” alisema.

Alifafanua kuwa mwakani kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa, mwaka 2015, unafanyika uchaguzi mkuu hivyo Katiba hiyo haiwezi kuwa imepatikana.

“Kongamano hili litakuja na mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na kufikisha kilio hiki kwa Rais ili tushauriane naye kitatokea nini kama Katiba Mpya itakuwa haijapatikana katika chaguzi hizi, kama ikiwezekana turekebishe maeneo yanayohusu uchaguzi katika Katiba ya sasa maana maoni yake yameshatolewa na wananchi.”CHANZO MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate