Rais wa Somalia alikuwa akikaribia kuwasili katika mji
wa bandari wa Marka kusini mwa Mogadishu mji mkuu wa Somalia wakati
wanagambo wa al Shabab walipourushia msafara wake maguruneti.
Abdikadir
Mohamed, Kamanda wa polisi ya Somalia amethibitisha kutokea shambulio
hilo na kueleza kuwa Rais Hassan Sheikh Mahmoud amewasili salama
salimini humo Marka umbali wa kilomita 90 kutoka Mogadishu.
Wanamgambo wa al Shabab wamesema wamewaua wanajeshi kadhaa na
kuharibu magari mawili ya kijeshi yaliyokuwa kwenye msafara wa Rais wa
Somalia ambao ulikuwa ukisindikizwa na askari jeshi wa kulinda amani wa
Umoja wa Afrika na wa serikali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment