Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyokwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013
Pichani ni sehemu ya wakazi wa Mkoa Iringa na vitongoji vyake wakiwa
wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013
linaloendelea kufanyika hivi sasa katika uwanja wa Samora.
Mmoja
wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz
akiwaimbisha mashabiki wake kwenye uwanja wa Samora,ambapo
tamasha la Serengeti fiesta linafanyika usiku huu.
Moja
ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake
Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa
Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti
fiesta likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
Msanii
aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba
jukwaaniwakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea
kwenye uwanja wa Samora.
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Samora.
Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga.
Ni noma saana
Anaitwa
Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa
Bongofleva akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe za mashabiki zikivuma
kila kona ya uwanja.
Anajiita
Rais wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha
mashabiki wake kwenye tamasha la
serengeti fiesta 2013,linalofanyika ndani ya uwanja wa Samora mkoani
Iringa.
Mmoja
wa madansa machachari sana kutoka THT,aitwaye Msami akiwa amebebwa juu
na mashabiki baada ya kuonesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma
jukwaani.
Wasanii
wanaokuja juu katika anga ya muziki wa kizazi kipya-hip hop.Stamina na
Young Killer wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku mayowe yakiwa
yametawala kila kona ya uwanja.
No comments:
Post a Comment