Msanii
wa Hip hop, Nick wa Pili akiwapanua mawazo wakazi wa Morogoro na kuwapa
mbinu zaidi za kutumia fursa zilizopo mkoani hapo.
Meneja Ujasiriamali wa Zantel, Haidar Chamshama, akiwaonyesha wakazi wa
Morogoro namna ya kutumia fursa ya kubana matumizi kwa upande wa
utumiaji wa simu za mkononi na kujua faida za simu zaidi katika
kujikwamua kimaisha.
Mkuu
wa Utafiti wa Maxcom Africa, Ahmed S Lussasi, akiwafafnulia wakazi wa
Morogoro namna wanavyoweza kufaidika na bidhaa za Maxcom katika
kujikwamua kimaisha.
Mtangazaji wa Kipindi cha Sport Extra cha Clouds FM, Shaffih Dauda akionyesha namna ya kutumia fursa kwa upande wa michezo.
Mbunifu
wa Mavazi wa Morogoro, Diana Magesa (kushoto), akizungumzia fursa ya
mambo ya ubunifu, huku akionyesha mavazi yake kwa kumvisha Mtangazaji wa
kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Jelard Hando, ambaye
alikuwa mshereheshaji wa semina hiyo.
Mtalaam wa mambo ya Kilimo, Yona Joram, akiwafafanulia namna ya kutumia fursa kwenye upande wa kilimo.
Mwakilishi
wa NSSF kutoka Makao Makuu, Salim Khalfani akizungumzia namna ya
kutumia fursa zinazotokana na mafao ya NSSF kwa wakazi wa Morogoro leo
ndani ya ukumbi wa Midland Hoteli mjini Morogoro.
Ruge
akihitimisha Semina hiyo kwa kukaribisha maswali kutokana na mafunzo
waliyoyapata wakazi wa Morogoro waliohudhuria kwenye semina ya Kamata
Fursa Twenzetu mapema leo.
Baadhi
ya wakazi waliokuwa ndani ya ukumbi huo wakiwa wamesimama baada ya
kuombwa kuimba wimbo wa Tanzania na Mrisho Mpoto kabla ya kuanza
kuonyesha fursa kupitia sanaa yake ya muziki.
Msanii
wa kughani mashairi, Mrisho Mpoto akiwaimbisha wimbo wa Tanzania wakazi
wa Morogoro muda mfupi kabla ya kuanza kutoa njia za kutumia fursa
kupitia sanaa ya muziki.
SEMINA ya Kamata Fursa Twenzetu inayotolewa na timu ya Serengeti
Fiesta 2013, kila mkoa inapotoa burudani, leo imeendelea tena kujenga na
kupanua mawazo ya wakazi wa Morogoro katika mpango wa kuwawezesha kujua
namna ya kutumia fursa zilizopo mkoani hapo katika kujikwamua kwenye
maisha yao.Semina hiyo ilifanyika mapema leo katika Ukumbi uliopo katika Hoteli ya Midland mjini Morogoro, ambapo baadhi ya wataalam kutoka sehemu mbalimbali walipata muda wa kuzungumza na wakazi hao na kuwajenga kwa kuwaonyesha njia mbalimbali za kujikwamua kimaisha.
(HABARI/PICHA:MUSA MATEJA/GPL, MOROGORO)
No comments:
Post a Comment