DUNIA imefika pabaya! Mrembo Yusta Mkali, mkazi wa Kawe, Dar ambaye
alikuwa mke wa mtu anadaiwa kuuawa kwa kutobolewa koromeo na mumewe,
Musa Senkando na kusababisha simulizi ya kutoa machozi kisa kikielezwa
kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Mauaji hayo ya kikatili yalitokea wiki iliyopita maeneo ya Kanisani
Kawe, Dar usiku wa kuamkia Ijumaa ambapo mwili wa marehemu ulikutwa
ukiwa na jeraha kwenye koo huku mwanaume huyo akiwa hajulikani aliko
baada ya kufanya mauaji hayo.
Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa Musa alikuwa akimfanyia visa mkewe huyo mara kwa mara ambapo mwaka jana alimpiga na kumchana mkono.
Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa Musa alikuwa akimfanyia visa mkewe huyo mara kwa mara ambapo mwaka jana alimpiga na kumchana mkono.
Ilidaiwa kuwa aliwahi kumpiga na stuli lakini alijikinga kwa mkono ili asiumie sehemu za kichwani.
Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa muuaji alitumia kitu chenye ncha kali ambacho alimshambulia nacho kwenye koromeo.
Marehemu ameacha mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Joshua Zebedayo.
Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa muuaji alitumia kitu chenye ncha kali ambacho alimshambulia nacho kwenye koromeo.
Marehemu ameacha mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Joshua Zebedayo.
Ilielezwa kuwa Joshua ndiye aligundua kuwa mama yake amekufa baada ya
kuingia chumbani kwa lengo la kufanya usafi lakini alishangaa kumuona
mama yake akiwa amelala huku amefunikwa shuka na alipojaribu kumuita
hakuitika ndipo akamfunua na kukutana na mwili ukiwa umejaa damu.
Mtoto huyo alipiga kelele akiomba msaada ambapo watu walijaa na kushuhudia mwili wa mwanamke huyo na kusababisha vilio kutawala.
“Huu ni unyama wa ajabu sana. Haya mapenzi ni ya kuyatazama sana. Ona
sasa mwanaume amemuua mkewe. Inauma sana,” alisema mama Jack ambaye ni
jirani wa familia hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar, Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mwili wa mwanamke huyo ulihifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyama na mtuhumiwa anasakwa kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mwili wa mwanamke huyo ulihifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyama na mtuhumiwa anasakwa kujibu tuhuma zinazomkabili.
Ilikuwa ni simanzi na majonzi wakati wa kuaga mwili wa marehemu Yusta, jana katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi.
CHANZO GLP
No comments:
Post a Comment