Washiriki
wa mkutano wa tamasha la jinsia tanzania 2013 wakiandamana kuingia
katika viwanja vya TGNP kabla ya kuanza kwa maadhimisho. Maadhimisho
hayo yanaenda sambamba na kusherehekea miaka 20 ya harakati za ukombozi
wa mwanamke kimapinduzi za mtandao huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Bi. Ussu Mallya akizungumza kuwakaribisha wageni
mbalimbali katika tamasha hilo na kutoa machache juu ya miaka 20 ya
harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi za TGNP.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Bi. Mary Rusimbi akizungumza kwenye mkutano wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2013.
Baadhi
ya wageni kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za kimataifa
wakifuatilia matukio anuai katika Tamasha la Jinsia Tanzania2013.
Watu wenye ulemavu wa kusikia wakielezewa kwa kutumia ishara masuala anuai yanayiowasilisha katika tamasha.
Wakati
mwingine burudani zilipozidi washiriki walishindwa kuvumilia na
kujikuta wakiingia kati na kusakata rumba. Vikundi mbalimbali vya muziki
na sanaa vilikuwa vikiburudisha.
Washiriki kutoka mikoa anuai wakijisajili kabla ya kuanza ushiriki wa Maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Tanzania Jijini Dar es Salaam
Kundi la wasanii wa Parapanda wakifanya igizo kuonesha jamii ya wanawake inavyonyanyasika katika maeneo ajira.
Mmoja wa wasanii akighani ngonjera katika maadhimidho hayo.
Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment