Rais wa Ufaransa Francois
Hollande ametaja makubaliano kati ya Marekani na Urusi kuhusu silaha za
kemikali za Syria kama hatua muhimu katika suluhu kubwa zaidi la mgogoro
wa kisiasa unaokumba taifa hilo.
Lakini kwenye hotuba yake bwana Hollande
aliongeza kusema kuwa "lazima wazo la kuchukulia Syria hatua za kijeshi
lisalie , la sivyo hapatakuwa na shinikizo.’’
Aidha Bwana Hollande alisema huenda
nchi wanachama wa baraza hilo wakakubaliana kuhusu kura katika baraza la
usalama la umoja wa Mataifa kwa azimio kuhusu Syria.
Holland anatarajiwa kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry hii leo kujadili swala hilo.
Rais huyo amesema kuwa sharti Syria iwekewe
vikwazo ili iharibu silaha zake za kemikali ikiwa itakataa kufuata
maagizo na matakwa ya mataifa ya nchi za kigeni.
"Ni muhimu kuongeza kwa haya yote tisho la
kuiwekea Syria vikwazo ikiwa makubaliano na malengo ya baraza la usalama
ya Umoja wa Mataifa hayatatimizwa,’’ aliongeza kusema Rais Hollande"Lakini hatua inayofuata ni kutafuta suluhu la kisiasa kwa haya yote.’’
CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment