EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 12, 2013

Ufisadi Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam.

Dar es Salaam: 
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilikiuka taratibu za utoaji wa zabuni ya kubomoa jengo lililokuwa ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani kilichopo Ubungo (UBT), ambalo lilianguka mwanzoni mwa mwaka huu na kusababisha madhara kwa watu na mali. 


Januari 21 mwaka huu, watu wanne walijeruhiwa baada ya magari yao waliyokuwa wameyaegesha katika eneo la UBT kuangukiwa na ukuta, huku magari 24 na bajaji nne zikiharibika vibaya.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa Kampuni ya Makalla Contractors Ltd ndiyo iliyofanya kazi ya ubomoaji huo, lakini hakukuwa na mkataba wa kazi hiyo baina yake na Jiji la Dar es Salaam.

Uchunguzi zaidi unaonyesha kuwa, licha ya kutokuwa na mkataba, Makalla Contractors Co. Ltd wamepeleka kwa uongozi wa jiji hilo madai ya Sh59, 615, 252 wakitaka walipwe kutokana na kazi hiyo.

“Makubaliano yalifanyika kwa mdomo na kazi ikaanza, hakukuwa na uitishwaji wa zabuni wala kufanyika taratibu zozote za kisheria, walipeana kazi hiyo kirafiki na baada ya jengo kubomoka ndipo walianza kuhaha jinsi ya kuwezesha kulipa fedha hizo,” kilisema chanzo chetu.

Katika moja ya nyaraka za kampuni hiyo kwenda Halmashauri ya Jiji, Kampuni hiyo ya Makalla inasema ilipewa kazi hiyo kutokana na gharama zake kuwa za chini na kwamba iliombwa kuanza kuitekeleza haraka kutokana na udharura wake kwa ahadi kuwa taratibu nyingine za kupewa LPO na mkataba zingefuata. Hata hivyo, taratibu za zabuni zinataka kazi itangazwe na hata kama kungekuwa na dharura ilipaswa kufuata utaratibu wa ‘single sourcing’ ambao ungewezesha kuchagua kampuni ya kutekeleza jukumu bila kuchelewa. 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusaini mikataba kwa niaba ya jiji hilo alisema: “Sijawahi kusaini mkataba unaohusu kampuni hiyo unayoitaja (Makalla) na wala sijawahi kusaini mkataba kuhusu ubomoaji wa pale Ubungo.” Alipobanwa akitakiwa aeleze sababu za ubomoaji kufanywa bila yeye kuhusishwa alijibu: “Waulize watendaji wa Jiji, muulize mkurugenzi maana huo ni wajibu wa watendaji na siyo wajibu wa Meya, nilichokwambia ni kwamba mimi sijasaini mkataba wowote kuhusu suala hilo.”


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alipoulizwa alisema hawezi kutoa taarifa kuhusu suala hilo kwenye vyombo vya habari.

“Wewe hizo taarifa umezipata wapi?... Mimi siwezi kukwambia mkandarasi gani aliyehusika, sitoi taarifa hizo kwenye vyombo vya habari… unazitaka za nini? Wananchi ndio wamekutuma uwatafutie taarifa? Wao wanatakiwa wasubiri huduma ikamilike, lakini siyo kumjua mkandarasi, kalipwa au hakulipwa,” alisema Kabwe.
Malipo kwa Mkandarasi

Wakati Kabwe akihoji maswali lukuki, habari zaidi zinasema ofisi yake imekuwa katika harakati za kuwezesha Kampuni ya Makalla kulipwa, na kwamba kinachokwamisha malipo hayo ni kutokuwapo kwa mkataba wa kazi. Fedha za ubomoaji kiasi cha Sh63 milioni zilitolewa na Ofisi ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na kuhamishiwa kwenye akaunti za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lakini imebainika kuwa kumekuwapo na harakati za fedha hizo kurejeshwa DART.

“Ofisi ya mkurugenzi inaendelea na mchakato wa kurejesha fedha hizo DART ili Kampuni ya Makalla ikalipwe huko maana ni ngumu malipo kufanyika hapa kwetu kwa sababu hakuna documents (nyaraka) za mkataba wa kazi, huwezi kulipa, sasa huko DART nao sijui watafanyaje,”kilidokeza chanzo chetu katika ofisi za Jiji. Hata hivyo, Ofisa Mwandamizi wa DART, Jack Meena alisema suala hilo linawahusu Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) na Halmashauri ya Jiji ambao ndiyo wamiliki wa kituo hicho.
“Sisi kazi yetu ni kuhakikisha eneo la mradi linakuwa tayari kwa ajili ya ujenzi. Kwa hiyo tulifanya tathmini na kulipa fidia na kumwachia mkandarasi,” alisema Meena.
Msimamizi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka katika Tanroads, Barakaeli Mmari alisema suala hilo linashughulikiwa na Halmashauri ya Jiji, hivyo waulizwe wenyewe.

“Ni kweli tunasimamia mradi wa mabasi yaendayo haraka, lakini suala la ubomoaji ni la Halmashauri ya Jiji. Wao ndio wanafahamu mkandarasi na kama alilipwa au hakulipwa,” alisema Mmari.
Sheria za Ubomoaji

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Kampuni ya Makalla iliandikiwa barua na Bodi ya Usajili wa Makadarasi (CRB), ikitakiwa kutoa maelezo ya kuhusika kwake katika kazi hiyo, pia vielelezo vilivyoonyesha jinsi kazi ilivyofanywa. CRB katika barua yake ya Mei 9, 2013 kwenda kwa Mkurugenzi wa Makalla Contractors Co. Ltd ambayo gazeti hili limeiona, ilitaka kampuni hiyo kuwasilisha mkataba wa kazi, majina ya wataalamu walioshiriki katika kubomoa jengo hilo na nyaraka za uthibitisho wa malipo yao.

Msajili wa CRB, Boniface Muhegi alikiri kwamba Kampuni ya Makalla imesajiliwa. “Halmashauri ya Jiji ndiyo waliomwajiri, ila kulipotokea malalamiko ndiyo tukawauliza (Jiji) wakakiri kwamba ndiye aliyefanya kazi hiyo,” alisema Muhegi na kuongeza:

“Mwanzoni kulikuwa na ubabaishaji. Tulipouliza tuliambiwa wenye magari waliambiwa wayaondoe kwanza… hilo ni tatizo la Jiji, lakini tutaichukulia hatua Kampuni ya Makalla kwa sababu imesababisha uharibifu wa mali za watu na kwa kutokuzingatia vigezo vya usalama kazini.” 

“Katika tathmini zetu tuna alama, kama zikifikia 60 au 70 tunatoa adhabu kulingana na kosa. Inaweza ikawa onyo, kusimamishwa kwa muda au kufutwa kabisa. Kwa kuwa hili ni kosa la kwanza tutaangalia vigezo vyetu,”alisema Muhegi.
Septemba 4, mwaka huu gazeti hili liliwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, 

Makalla Moseka ambaye awali alisema taarifa zote kuhusu suala hilo zinapaswa kutolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, lakini baadaye alimtaka mwandishi afike ofisini kwake kesho yake kwa maelezo zaidi.

Gazeti hili lilifika katika ofisi hizo, chumba namba tisa cha ghorofa ya 10 katika Jengo la Ushirika, Lumumba, lakini ofisi hizo zilikuwa zimefungwa, huku majirani zake wakisema kuwa ofisi hiyo imefungwa muda mrefu.

Baada ya kumkosa, mwandishi alimpigia simu siku hiyo ya Septemba 5 ambapo Makalla alikanusha kwamba kampuni yake iliwahi kufanya kazi ya aina hiyo.

“Sikiliza bwana, mimi sikuhusika na kazi hiyo, inawezekana kuna watu walishafanya kazi kwenye kampuni hii, halafu wakaenda kufanya kazi kwa jina la kampuni yangu,” alisema Makalla.

Baada ya kubanwa zaidi, Septemba 7, Makalla aligeuka na kukiri kuhusika na kazi hiyo, huku akitaka mwandishi aonane naye Septemba 8. Alipotafutwa siku hiyo, alisema kwamba yuko msibani, hivyo kuahidi kwamba angekuwa tayari kuzungumza Septemba 10.

Gazeti hili lilimtafuta juzi na jana, lakini mara zote alipopigiwa simu alikuwa akikata baada ya mwandishi kujitambulisha.
CHANZO CHA HABARI NA GAZETI LA MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate