Dar es Salaam.
Wanafunzi 868,030 wa Darasa la Saba wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Jumatano na Alhamisi wiki hii, ikiwa ni mwanzo wa mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa utakaotekelezwa kwa kuanzia katika mitihani hiyo.

Taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), inaonyesha kuwa wanafunzi hao wanatoka kwenye shule 15,677 zikiwamo za umma na binafsi.
Inaeleza taarifa hiyo kuwa, wanafunzi
wanaotarajiwa kufanya mtihani wa lugha ya
Kiswahili ni 844,810 kati yao wasichana wakiwa 444,475 na wavulana 400,335. Kati ya wanafunzi hao, wasioona ni 88 wavulana wakiwa ni 56 na wasichana 32 huku wenye uono hafifu wakiwa 546 na kati yao wavulana ni 263 na wasichana 283.

Watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya
Kiingereza ni 22,535 na kati yao wavulana wakiwa 11,430 na wasichana
11,105. Wanafunzi wenye uono hafifu kati ya hao ni 51, wavulana
wakiwa 21 na wasichana 30.
Mwaka jana wanafunzi 894,881 kutoka shule 15,363 walifanya mtihani huo, huku wale waliofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili wakiwa 873,837 wavulana walikuwa 415,572 na wasichana 458,265.
Waliofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza
walikuwa 20,457 wavulana wakiwa 10,422 na wasichana 10,035. Wenye uono
hafifu walikuwa ni 45 wavulana wakiwa 26 na wasichana 19.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi, alilieleza gazeti hili kuwa tayari mitihani imeshasambazwa huku akionya kuhusu wale watakaojaribu kufanya udanganyifu wa aina yoyote ile.
“Tunawataka wanafunzi na wadau wote wanaohusika
na mtihani huu, wasije wakajihusisha na udanganyifu kwa namna yoyote
ile, Necta tupo makini na tumejipanga kwa chochote kitakachotokea,”
alisema na kuongeza:
“Tunaamini kuwa wanafunzi wameandaliwa vya kutosha na wao ni vyema wajiandae zaidi kisaikolojia, yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu tutamchukulia hatua zinazostahili ikiwa ni pamoja na kumfutia matokeo.”
Wanafunzi hawa wanaanza mtihani wakati ambapo
Serikali imeweka lengo la kuinua ufaulu wa mtihani huo kutoka asilimia
31 za mwaka jana mpaka 60 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Maandalizi ya mwisho
Shule mbalimbali za msingi zimeshafungwa tangu
Ijumaa iliyopita kati ya wiki moja hadi mbili zikiwaacha wanafunzi wa
darasa la saba wakikamilisha hatua za mwisho mwisho kabla ya kufanya
mtihani wao.Akizungumza jana kwa simu, Mwalimu Mkuu wa Shule ya High Mount
iliyoko Guluka Kwalala Kata ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, George
Mgombozi alisema: “Kwa sasa tunawajenga wanafunzi kisaikolojia baada ya
kuwapika vya kutosha. “Kimsingi, tunachowaambia wanafunzi ni kwamba
watambue kuwa wanapofanya mitihani yao waone kama mitihani ya kawaida tu
wanayoifanya kila siku,” alisema.
Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mloganzila iliyoko Wilaya Kisarawe Mkoa wa Pwani, Grace Msele amewataka wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kutumia siku mbili zilizobaki kujiandaa kisaikolojia na kujiepusha na michezo ya hatari kabla ya kuanza mitihani yao. Akizungumza kwenye kikao cha wazazi shuleni hapo juzi, Msele alisema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki ili kuwajengea uwezo.

No comments:
Post a Comment