WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Hussein Mwinyi leo ameongoza maelfu ya waandamanaji katika maandamano ya amani ya kupiga vita kansa ya matiti kwa wanawake nchini na kutoa mchango wa shilingi 10,000,000 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Dk.Mwinyi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye harambee hiyo ya kusaidia udhibiti wa kansa ya wanawake nchini iliyoendeshwa na Taasisi ya Kudhibiti Kansa ‘ORCI’ chini ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar iliyofanyika SIKU YA JANA katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar na kuhudhuriwa na waandamanaji mbalimbali nchini, akisoma hotuba ya Mhe. Pinda.
“Waziri mkuu anaungana na Taasisi ya Kansa nchini ‘ORCI’ hiyo japo hakufika na amechangia shilingi milioni 10, na amewataka wanawake nchini kuchukua tahadhari mapema juu ya tatizo la kansa ya matiti, hii ni pamoja na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara juu ya Afya zao,” alisema Dk Mwinyi.
Hata hivyo Mkuu wa shughuli hiyo Dr.Julius Mwaiselage amesema anapongeza mwamko na hamasa kubwa aliyoutoa Staa wa sinema za kibongo Jackob Steven ‘JB’ kwa kuchangia Shilingi Milioni 2.
Wadau wameombwa kuchangia Mfuko wa Hospitali ya Ocean Road kwa M-PESA namba Namba 175555.
(NA JELARD LUCAS GLP)
No comments:
Post a Comment