Zeidan alitoa wito kwa Marekani kusaidia Libya kupambana na wapiganaji wa kiisilamu
Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan
aliyeripotiwa kutekwa nyara na waliokuwa waasi katika jiji kuu la Libya
Tripoli mapema hivi leo ameachiliwa.
Maafisa wamenukuliwa wakisema kuwa hakuumizwa.
Tukio hilo limeshutumiwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.
Ali Zeidan alitekwa nyara na kundi la waasi waliokuwa na uhusiano na serikali kwa jina Revolutionaries Operations Room.
Walisema walimteka nyara kwa maagizo ya mwendesha mkuu wa mashitaka ingawa wizara ya sheria imekanusha madai hayo.
Kundi hilo lilikuwa miongoni mwa makundi ya
wapiganaji walioghadhabishwa na hatua ya makomando wa Marekani kumkamata
Anas Al-Liby mshukiwa wa kundi la kigaidi la al-Qaeda .
Wengi walitaja hatua ya Marekani kama ya
kuingilia uhuru wa taifa hilo na hata kutaka maelezo kutoka kwa balozi
wa Marekani nchini humo.
Picha ya Zeidan akitekwa nyara mjini Tripoli
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.
Serikali imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kali
baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa viongozi wa al-Qaeda
Anas al-Liby nchini Libya.
Bwana Liby alikamatwa Jumamosi mjini Tripoli kwa
madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya
balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2008.
Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.
Kwa upande wake Zeidan alitoa wito kwa Marekani
na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha vitendo vya
wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi yake inatumia
kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya
kanda hiyo.
No comments:
Post a Comment