MSANII wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa sasa
hivi anaiogopa na kuiheshimu sana pombe akiamini kwamba ndiyo chanzo cha
maisha kuharibika.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Lulu alisema tangu ametoka
gerezani ameamua kujiweka pembeni na kilevi hicho na kwamba bora aitwe
mshamba.
“Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo
kichocheo cha kila baya hapa duniani, watakaoniona mshamba kwa
kubadilika kwangu wanione hivyohivyo,” alisema Lulu.

Msanii
huyo kipindi cha nyumba alikuwa hakamatiki kwa kilevi na kuna wakati
aliwahi kuzimika alipofakamia pombe za ofa alipokuwa ndani ya Ukumbi wa
Maisha Club, jijini Dar.
No comments:
Post a Comment