MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Frola Mtegoa ameibuka na kueleza
kuwa, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mkwe sahihi kwake kwa namna alivyo na
heshima na anavyomjali kama mama yake.
Akizungumza wikiendi iliyopita nyumbani kwake, Kimara - Temboni, Dar,
mama huyo alisema, kama mwanaye angekuwa hai angekuwa amepata mke bora
wa maisha yake, naye pia alikuwa na mkwe sahihi.
“Najua mtoto wangu ametangulia mbele za haki lakini faraja anayonipa Lulu ni kubwa mno na najisikia furaha. Kama Mungu angemwacha Kanumba hai mpaka leo kwa kweli Lulu angekuwa mkwe bora sana kwangu.
“Najua mtoto wangu ametangulia mbele za haki lakini faraja anayonipa Lulu ni kubwa mno na najisikia furaha. Kama Mungu angemwacha Kanumba hai mpaka leo kwa kweli Lulu angekuwa mkwe bora sana kwangu.
“Sina jinsi, ndiyo imeshatokea lakini mimi kama mzazi bado
nitaendelea kumpenda na kuwa bega kwa bega na Lulu hata akipata mchumba
mwema wa kumuoa, sina tatizo na hilo... namwombea sana kwa Mungu huyu
binti,” alisema kwa hisia mama Kanumba.
No comments:
Post a Comment