MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amejikuta katika wakati
mgumu baada ya kukutana na mila za kabila la mumewe mtarajiwa, Dickson
mwenye asili ya Musoma Vijijini, mkoani Mara.
Shamsa Ford.
Akizungumza na mwandishi wetu ndani ya Viwanja vya Leaders Club
Kinondoni jijini Dar, msanii huyo alisema alikutwa na magumu hayo
mwishoni mwa mwezi uliopita alipokwenda kutambulishwa ukweni huko.

Alisema,
tofauti na alivyozoea, alilazimika kupika ugali mkubwa wa kulisha zaidi
ya watu thelathini, kuchanja kuni porini, kufuata maji umbali wa
kilometa tatu kutimiza wajibu wa mwanamke.
“Ilikuwa balaa, nilikutana na wakati mgumu sana ukweni, kupika ugali
mkubwa, halafu ugali wenyewe ni wa mtama na muhogo, si mchezo,” alisema
Shamsa.
No comments:
Post a Comment