“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na
taarifa za kifo cha Mke wako, Mama Martha Peter Lubuva aliyekuwa
amelazwa katika Hospitali ya Apollo nchini India akipatiwa matibabu ya
ugonjwa wa Kisukari ambao umesumbua kwa muda mrefu”, amesema Rais
Kikwete katika salamu zake za Rambirambi.
Rais Kikwete amesema anatambua fika machungu ambayo hivi sasa
wanapitia watoto na Familia nzima ya Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva
kutokana na kuondokewa na Mama yao Mzazi na
Kiongozimuhimu wa
Familia, lakini amewaomba wawe watulivu na wavumilivu, lakini muhimu
zaidi wawe na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo
ya mpendwa wao.
“Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nayi katika kuomboleza msiba huu
mkubwa na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza
Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Mama Martha Peter Lubuva kwa
kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola”.
Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
DAR ES SALAAM.
18 Januari, 2014
No comments:
Post a Comment